Saturday, November 28, 2009

Magufulu kulamba PhD leo

Waziri wa maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli, leo anatarajiwa kuwa miongoni mwa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam watakaohitimu masomo ya Udaktari wa falsafa, yaan PhD katika kemia.
Tumpongeze Magufuli, sit u kwas kuhitimu, bali kuhitimu katiak fani ya sayansi ambayo wengi tunaiona kuwa ni ngumu

Tuesday, November 17, 2009

Waliokuwa wabunge wa CUF waachiwa huru, wakamatwa tena

Wale waliokuwa wabungew a CUF ambao mwaka 2004 walishtakiwa kwa kosa la kughushi vyeti vya ndoa, wameachiwa huru na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo lakini wakakamatwa tena muda mfupi baadaye.

Haijaeleweka mara moja ni kwa nini wabubnge hao wamekamatwa ingawa inaaminika kuwa Jeshi la Polisi lina lengo la kuunda upya mashtaka dhidi yao na kuwafikisha tena mahakamani.

Haijulikani iwapo Wabunge hao, pamoja na watu wengine wane akiwmo ofisa uhamiaji na mashehe waliowafungusha ndoa bandia watafikishwa tena au la.

Wabunge hao ni Khamis Ally Salehe aliyekuwa Mbunge wa Magogoni na Khalifa Mohamed Issa aliyekuwa mbunge wa Mtambwe. Majimbo haya yote yako Pemba.

Wengine wanaliokuwa wameshtakiwa pamoja na wabunge hao ni mashehe watatu kutoka msikiti wa Ilala Bungoni ambao ni Abdul Wakati, Abdallah Matulanga na Khamis Mwinshehe pamoja na ofisa uhamiaji, Augustino Haule.

Waliachuwa huru na hakimu mkazi Aniseta Wambura baada ya mwendesha mashtaka kusema kuwa hakuwa na dhamira ya kuendelea na kesi hiyo. Lakini wakati wa usikilizaji wa awali wakesi, upande wa mashitaka ulidai mwezi Agosti kuwa utaleta mashahidi 20 lakini hadi watuhumiwa hao wanaachiwa, ni shahidi mmoja tu ndioye alifika mahakamani hapo kutoa ushahidi.
Wabunge hao wanadaiwa kughshi hati za ndoa zinazoonyesha kuwa Salehe alikuwa amefunga ndoa na Fardhosa Mohamed na Issa alikuwa amefunga ndoa na Sophia Rage. Wanawake hao wote wanadaiwa kuwa ni wasomali.

Lakini wabunge hao wa zamani wanadaiwa pia kulidanganya Bunge kuwa wanataka kwenye Ujerumani na wake zao hao huku wakijua kuwa si wake zao halali. Inadaiwa kuwa walikuwa na lengo la kuwasaidia wanawake hao kufika Ujerumani kwa ajili ya kuomba hifadhi kama wakimbizi.

Tuesday, November 10, 2009

TRA yakamata mitambo ya Dowans

Mamlaka ya mapato Nchini-TRA-imekamata vifaa mbalimbali vya kampuni ya kufua umeme ya Dowans kwa madai ya kutoli[pa kodi inayozidi Sh bil 9. Vifaa hivyo vimekamatwa na wakala wa TRA ambaye ni Majembe Auction Mart leo asubuhi. kampuni hiyo imeitaka Dowans kulipa kodi hiyo katika kipindi cha siku 10 la sivyo mali zake zitapigwa mnada.
Dowans ni kampuni ambayo ilinunua mkataba kutoka kwa Richmond, iliyokumbwa na kashfa ya kusema uongo ili kujipatia mkataba wa kuzalisha megawati 100 za umeme wa dharura na kuiuzia Tanesco.
Mkataba wa Dowans ulifutwa mwaka jana na serikali baada ya kubanini kwua Richmond ilikuwa imesema uwongo wakati wa kutafuta mkataba huo

Rostam aendeleza mjadala wa Richmond

Mbunge wa Igunga bado hajakubaliana na ripoti ya Richmond na sasa anataka iundwe tume maalum ya majaji kulichunguza suala hilo upya. Anasema iwapo tume hiyo ya majaji itabaini kuwa amehusika wka namna yoyote katika kashfa hiyo, basi afukuzwe kwenye nyadhifa zote alizonazo ndani ya chama na kisha kuchukuliwa hatua za kisheria.
Rostam amezidi kusisiza kuwa ripoti ya Richmond iliyowasilishwa bungeni ya mwenyektii wake Dk Mwakyembe kuwa ilijaa uongo dhidi yake.
Je, atafanikiwa katika jitihada hizi mpya za kutaka kujitakasa?

Thursday, November 5, 2009

Richmond yaota mbawa Bungeni

Kuna uwezekano mdogo sana wa Bunge linalomaliza kikao chake Jumamosi kujadili ripoti ya serikali kuhusu utekelezajiw a maazimio ya Bunge yaliyomo kwenye ripoti ya Bunge iliyotolewa mwaka jana.
Ratiba zilizotolewa hapa Bungeni zinaonyesha kuwa hakuna majadiliano kuhusu ripoti hiyo kama ilivyokuwa inadatarajiwa. Kamati ya Nishati na Madini haina ratiba ya kujadili ripoti hiyo ambayo waziri aliahidi kuipatia hapa Dodoma. Na waziri mwenye wala hayupo Dodoma