Monday, November 5, 2007

Kunani NEC?

Habari zinakuja toka Dodoma hivi sasa kuwa baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa, wapo waliozimia na wengine kuangusha vilio kama watoto wadogo. Hivi walipokuwa wanagombea hawakujua kuwa kuna kushindwa? Au walishajihakikishia ushindi? Kama ndio hivyo, sasa hiyo inayoitwa demokrasia ipo wapi?
Kwanza wanalilia nini? NEC yenyewe hukutana kama mara nne kila mwaka, hata kama posho yake ni sh 100,000 kwa siku, hivi vipesa hivyo ambayo wanalipwa kama posho vinalingana na mamilioni ambayo wameyatumia kufanya kampeni? Si afadhali wangebaki na mamilioni yao wakayatumbua kidogokidogo.
Kama hawalilii fedha, hivi kuna nini hasa kwenye NEC?

3 comments:

Anonymous said...

Hongera bwana Nyanje kwa kujumuika na hii technologia ya kisasa. Sisi kutoka huku Kenya tunakupa zetu hongera, tutashiriki kabisa na ukiona twalala sana, tuamshe. Tupe kiboko nasi tutaamka na kuchangia itakanavyo. Mambo mengi yanafanyika humu (Huu ni msimu wa kupiga kura) na hivyo ukiona tumepotea usijali sana.

Mzee wa Sumo said...

Sawa mzee tumekubali mambo yako makubwa, tunasubiri fitina zako Fisadi Kiongozi! Usiache tu kuweka mambo.

Unknown said...

Usipate shida mzee wa sumo, mambo yatawekwa sana,labda yasiwepo, lakini sidhani kama yanaweza kuisha.
Asante kwa kufika hapa
Nyanje