Jitihada za kuwazuia wafanyakazi wa Kampuni ya reli nchini kufanya mgomo zimegonga mwamba. Muda mfupi uliopita, wafanyakazi wa kampuni hiyo ambayo ilikodishwa na serikali mwaka huu, wametoa notisi ya saa 48 kwa mwajiri wao, awaongezee mshahara.
Iwapo mwajiri atashindwa kutekeleza ombi hilo, wafanyakazi hao wamejiandaa kufanya mgomo nchi nzima na madhara ya mgomo huo yanaweza kuhatarisha hali ya uchumi wa nchi na kusababisha mvugano katika jamii.
Hii ni kwa sababu Reli hiyo ndiyo tegemeo la usafiri kwa mikoa mingi ya bara hivyo iwapo itashindwa kufanya kazi kutokana na mgomo huo, kuna uwezekano mkubwa bidhaa nyingi zikakosekana katika mikoa kadhaa.
Sakata la wafanyakazi hao lilianza mara tu baada ya mkodishaji, kampuni ya rites ya India, alipoingia kuanza kazi mwanzoni mwa mwaka huu.
Baada ya kuja kwa mkodishaji huyo anayemiliki sehemu kubwa ya hisa za kampuni hiyo, wafanyakazi walitaka kulipwa mafao yaao ya miaka iliyopita na kuanza mkataba upya na mwajiri huyo.
Lakini madai hayo yalitawaliwa na mizengwe na kabla halijapatiwa ufumbuzi unaoeleweka, wafanyakazi walikuja na dai jingine wakitaka nyonmgeza ya mishahara.
Dai hilo la pili ndilo lililozaa notisi iliyotolewa jana na iwapo haitatekelezwa hadi Jumatano, wafanyakazi hao wamesema kuwa watagoma.
2 comments:
Huwa nikiangalia picha za treni india ambazo ni kawaida kuona watu wanasafiri mpaka juu ya mabehewa, huwa nasita sana kuamini kuwa hawa jamaa wa Rites ni suluhisho la shughuli za reli Tanzania.
Wakigoma kuna maeneo wanaweza hata kufa njaa:-(
Nadhani ni aina fulani ya ukoloni unarudi, lakini inauma sana kutawaliwa na wahindi!!!
Post a Comment