Katika kile kinachoweza kuelezewa kama aina fulani ya kuchafuana, watu kadhaa, walikubali kupoeka fedha kutoka kwa mfanyabiashara Yusuf Manji kwa ajili ya kuandaa kampeni za kumchafua mfanyabishara hasimu wake, Reginald mengi.
Lakini, Mengi inaelekea alikuwa na 'inteligence' ya nguvu kwani aliweza kupenyeza watu wake katika kikao cha timu hiyo na kufanikiwa kupata picha za video za mkutano huo na sehemu kubwa ya majadiliano.
Mkanda huo wa video ulionyeshwa katika kituo cha ITV kuanzia jana jioni na taarifa hiyo kurudiwa leo asubuhi.
Katika kampeni hizo, watu hao walikuwa wakipanga kueneza taarifa kuwa Mengi, ameamua kutumia fedha zake, kupiga vita utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Inadaiwa kuwa lengo la uzushi huo ni kumgombanisha Mengi ya rais Kikwete.
Kuna taarifa pia kuwa Mengi amefikisha nakala ya mkanda huo kwa Rais.
No comments:
Post a Comment