Wabunge wawili, Ibrahim Sanya (Mji Mkongwe-CUF) na Susan Lyimo (Viti Maalum-Chadema) wamehoji bungeni kuhusiana na mbwa aliyeuawa huko Tarime wakati wa kampeni.
Wakichangia muswada wa hali bora za wanyama uliowasilishwa leo asubuhi na John Magufuli (Waziri wa Uvuvi), wabunge hao walitaka kujua hatua zilizochukuliwa dhidi ya watu waliosika na tukio hilo.
Kwa upande wake, Sanya alisema kuwa kitendo cha kumvika mbwa huyo bendera ya CCM ni ujinga. Lakini aliongeza kuwa mtu aliyemuua mbwa huyo kutokana na kuvikwa bendera hiyo, ni mjinga mkubwa zaidi.
Suzan Lyimo, yeye ameitaka serikali kutoa mawelezo ya kina kuhusiana na tukio hilo.
Lakini wakati akihitimisha mjadala wa muswada huo, Magufuli alikataa kulizungumzia suala hilo kwa undani kwa maelezo kuwa hivi sasa hajui iwapo ilifunguliwa kesi mahakamani kuhusiana na tukio hilo au la.
No comments:
Post a Comment