Mmoja wa wahiriri wa gazeti la Kulikoni, Nyaronyo Mwita Kicheere, amejitosa kwenye mbio za kuwania Ubunge wa jimbo la Tarime kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Nyaronyo anakuwa mwanachama wa saba wa chama hicho kuchukua fomu hiyo kuwania kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Cha cha Wangwe, aliyefariki hivi karibuni kwa ajali ya gari eneo la Pandambili mkoani Dodoma. Wanachama wengine sita wamechukua fomu hizo wilayani Tarime, kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na Chadema, lakini Nyaronyo aliomba kuchukulia fomu hizo jijini Dar es Salaam na kukubaliwa. Nyaronyo alichukua fomu jana katika ofisi za Makao Makuu ya Chadema na kuaeleza kuwa ameamua kugombea nafasi hiyo, akisukumwa na dhamira inayomtaka sasa kusema moja kwa moja na wahusika bada ya kuona kauli zake anazoziandika katika magazeti hazipatiwi majibu. Alisema kuwa amekuwa akiandika mambo mengi katika magazeti, akijinasibu kuwa yeye alikuwa mwandishi wa kwanza kuandika masuala ya Richmond, lakini inaelekea viongozi hawasomi makala anazoziandika. Kwa hiyo, sasa anataka kupata nafasi ya kuzungumza moja kwa moja kupitia Bungeni. Nyaronyo aliwahi kuwa katibu wa Wangwe katika harakati za kusaka ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2005. |
Tuesday, August 26, 2008
Nyaronyo ataka kumrithi Chacha Wangwe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment