Mkuu Meshi ya ulinzi mstaafu Generali Robert Mboma amechukua fomu kuomba kugombea ubunge wa jimbo la Mbeya vijini huku akikanusha kuwa ametumwa na rais Kikwete kuwnia nafasi hiyo.
Anasema kugombea ubunge ni haki yake na kugombea nafasi hiyo yamekuwa ni maamuzi yake binafsi, hivyo isihesabiwe kuwa ameingia baada ya kushawishiwa na mtu yeyote.
Alisema anagombea nafasi hiyo si kwa ajili ya kutafuta utajiri, bali kuwasaidia wananchi wenzake wa mkoa wa Mbeya kuleta maendeleo.
Alisema kipaumbele chake kitakuwa ni kutatua kero za muda mrefu zinzowakabili wananvhi wa jimbo hilo kama vile ukosefu wa maji na huduma nyingine za jamii.
"Hakuna masilahi yoyote ambayo yamenishawishi kugombea nafasi hii kwani baada ya kustaafu nilipata kiiinua mgongo changu ambacho kinanitosheleza katika kuendesha maisha yangu hivyo nia yangu ni kuwakilisha mawazo, fikra na kero za wananchi ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo katika jimbo langu la Mbeya vijijini," alisema.
Hadi Ijumaa jioni, jumla ya wanachama tisa walikuwa wameshachukua fomu hizo. Hao ni Mchungaji Luckson Mwanjali, Michael Mponzi,Jjovita Diyami, Flora Mwalyambi, Alaan Mwaigaga, Petro Mwashusa, Maria Mwambanga na Andrew Sayila .
No comments:
Post a Comment