HII NI TAARIFA YA IKULU, KAMA ILIVYOTOLEWA:
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Januari 15, 2009, anaanza awamu ya pili ya mikutano muhimu na wizara mbalimbali kufuatilia utendaji wa wizara hizo, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, pamoja na maagizo aliyoyatoa kwa wizara hizo wakati anaingia madarakani.
Katika mikutano ya mwanzo, Rais Kikwete ataanza na wizara zinazohusika na masuala ya uchumi, ambayo ni sekta kuu lengwa katika utekelezaji wa Serikali ya Rais Kikwete kwa mwaka huu, 2009.
Leo katika mkutano wake wa kwanza ataanza na Wizara ya Miundombinu pamoja na uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam na Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL).
Kesho, Ijumaa, Januari 16, 2009, ataendelea na Wizara ya Miundombinu kwa kukutana na viongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Wizara yenyewe, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Wakala wa Majengo ya Serikali, TANROADS na SUMATRA.
Jumatatu ijayo, Januari 19, 2009, Rais atakutana na viongozi wa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA), Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Wizara ya Fedha na Uchumi pamoja na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).
Jumatatu ya Februari 9, 2009, Rais atakutana na viongozi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko; Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) pamoja na Bodi ya Biashara ya Nje (BET).
Jumanne, Februari 10, 2009, Rais atakutana na uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Kusambaza Umeme Vijijini (REA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).
Februari 11, 2009, Rais atakutana na uongozi wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika. Siku hiyo hiyo mchana, Rais atakutana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia; Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Alhamisi ya Februari 12, 2009, Rais atafanya kikao na Wizara ya Elimu, Mafunzo na Ufundi; Baraza la Mitihani, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, TAHLISO na viongozi wa vyuo vikuu vya umma nchini.
Ijumaa ya Februari 13, 2009, Rais atakutana na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Januari, 2008
No comments:
Post a Comment