Mamlaka ya mapato Nchini-TRA-imekamata vifaa mbalimbali vya kampuni ya kufua umeme ya Dowans kwa madai ya kutoli[pa kodi inayozidi Sh bil 9. Vifaa hivyo vimekamatwa na wakala wa TRA ambaye ni Majembe Auction Mart leo asubuhi. kampuni hiyo imeitaka Dowans kulipa kodi hiyo katika kipindi cha siku 10 la sivyo mali zake zitapigwa mnada.
Dowans ni kampuni ambayo ilinunua mkataba kutoka kwa Richmond, iliyokumbwa na kashfa ya kusema uongo ili kujipatia mkataba wa kuzalisha megawati 100 za umeme wa dharura na kuiuzia Tanesco.
Mkataba wa Dowans ulifutwa mwaka jana na serikali baada ya kubanini kwua Richmond ilikuwa imesema uwongo wakati wa kutafuta mkataba huo
No comments:
Post a Comment