Afya ya waziri Mkuu wa zamani na mwanasiasa mkongwe nchini, Mzee Rashid Mfaume Kawawa, bado si ya kuridhisha na amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Jana jioni ziliibuka habari za kutatanisha kutokana na uvumi kuwa Mzee Kawawa alikuwa amefariki dunia. Ukweli ni kuwa bado yuko mzima ingawa hali yake kiafya si njema sana.
Tuendelee kumuombea Simba wa Vita huyu arejee katika hali yake nzuri kwa sababu bado taifa linamuhitaji sana
No comments:
Post a Comment