Mzee rashid Kawawa amefariki leo majira ya saa 3.20 katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kutokana na matatizo ya figo na moyo. Alifikishwa hospitali hapo jana kutoka hospital ya usalama wa taifa uiliyopo Kijitonyama ambako asubuhi alikuwa amekwenda kufanyiwa check up ya malaria kabla hajasafiri. Ilikuwa ni kawaida yake kucheck afya kabla ya kusafiri.
Alipopimwa alionekana hana malaria na akaruhusiwa kurudi nyumbani. Lakini wakati wakiwa njuia, hali yake ilibadilika ghafla na akaishiwa nguvu. wakaamua kurudisha tena hospitali ambako vipimo vilionyesha kuwa kiwango cha sukari kilikuwa chini sana, karibu na sifuri.
Akakimbizwa Muhimbili ambako vipimo zaidi vilionyesha kuwa figo zake zote mbili zilikuwa zinmeacha kufanya kazi.
Aliongezewa kiwango cha sukari na hali yake ikatengemaa. Lakini asubuhi ya leo, kama saa 12 hivi, moyo nao ukaacha kufanya kazi. Madaktari walifanya jitihada za kuuamsha lakini ulikuwa ukiamka na kufanya kazi kwa muda na kisha kuacha tena kufanya kazi hadi saa 3.20 alipofariki.
Taratibu za mazishi zinafanywa kwa pamoja baina ya serikali na familia. rais Kikwete ametangaz wiki moja ya maombolezo ya kitaifa
No comments:
Post a Comment