Tuesday, January 27, 2009

Twin Tower za BoT zazaa kesi

maofisa wawili wa Benki Kuu (BoT), Amatus Joachim Liyumba na Deogratius Dawson Kweka wamefikishwa katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na shitaka la kutumia madaraka yao vibaya katika mradi wa ujenzi wa mirana pacha ya BoT na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilini bnilioni 221.
INgawa walikana mashitaka na upande wa mashitaka kutoweka pingamizi ya dhamana, lakini walishindwa kutekeleza masharti ya dhamana na hivyo kepelekwa katyika mahabusu ya keko hadi Februari 10 kesi hiyo itakapotajwa tena.
Liyumba na mwenzake wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya katika mkataba wa ujenzi huo na kuidanganya Bodi ya Wakurugenzi wa BoT ambayo ilifanya maamuzi yanayopingana na sheria ya manunuzi ya umma, wakati wa kuamua kuhusu mradi huo.
Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika lakini watuhumiwa walitakiwa kuleta mahakamani nusu ya kiasi cha fedha zilizotajwa (yaani sh bilioni 221). Kwa wastani, kila mmoja alitakiwa kuweka mahakamani si chini ya shilingi bilioni 50 au kutoa hati za mali zisizohamishika zenye thamani kama hiyo.
Wakili wa Liumba, Alexander Kyaruzi, aliiambia mahakama kuwa mteja wake ana hati tatu za nyumba ambay kila moja ina thamani ya sh milioni 600 lakini upande wa mashitaka waliomba muda ili kuzipitia hati hizo ilim kuthibitisha kuwa ni halali.
Thamani ya ujenzi wa majengo hayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi wengi, wakiwamo wabunge wa upinzani na vyombo vya habari, huku seriakli ikitoa majibu yasiyojitosheleza kuhalalisha ujenzi huo.
Suala hilo lilikuwa chini ya uchunguizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa muda mrefu.

Wednesday, January 14, 2009

Kikwete kutembelea wizara kwa awamu ya pili

HII NI TAARIFA YA IKULU, KAMA ILIVYOTOLEWA:


DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Januari 15, 2009, anaanza awamu ya pili ya mikutano muhimu na wizara mbalimbali kufuatilia utendaji wa wizara hizo, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, pamoja na maagizo aliyoyatoa kwa wizara hizo wakati anaingia madarakani.

Katika mikutano ya mwanzo, Rais Kikwete ataanza na wizara zinazohusika na masuala ya uchumi, ambayo ni sekta kuu lengwa katika utekelezaji wa Serikali ya Rais Kikwete kwa mwaka huu, 2009.

Leo katika mkutano wake wa kwanza ataanza na Wizara ya Miundombinu pamoja na uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam na Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL).

Kesho, Ijumaa, Januari 16, 2009, ataendelea na Wizara ya Miundombinu kwa kukutana na viongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Wizara yenyewe, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Wakala wa Majengo ya Serikali, TANROADS na SUMATRA.

Jumatatu ijayo, Januari 19, 2009, Rais atakutana na viongozi wa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA), Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Wizara ya Fedha na Uchumi pamoja na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).

Jumatatu ya Februari 9, 2009, Rais atakutana na viongozi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko; Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) pamoja na Bodi ya Biashara ya Nje (BET).

Jumanne, Februari 10, 2009, Rais atakutana na uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Kusambaza Umeme Vijijini (REA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).

Februari 11, 2009, Rais atakutana na uongozi wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika. Siku hiyo hiyo mchana, Rais atakutana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia; Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Alhamisi ya Februari 12, 2009, Rais atafanya kikao na Wizara ya Elimu, Mafunzo na Ufundi; Baraza la Mitihani, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, TAHLISO na viongozi wa vyuo vikuu vya umma nchini.

Ijumaa ya Februari 13, 2009, Rais atakutana na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA).

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

14 Januari, 2008

Tuesday, January 6, 2009

Heri ya Mwaka Mpya

Mwaka umeisha na tumeuanza mwingine. Nilipotea kidogo lakini nimerudi tena na nianze kwa kuwatakia nyote mnaolifuatilia jamvi hili gheri ya mwaka mpya. Matarajio yangu kwua huu utakuwa ni mwaka wa baraka na fanaka