Wednesday, November 14, 2007

Karibuni Arusha

Jamani, nipo katika mji wa kitalii wa Arusha. Nimewasili hapa jana majira ya saa 1 jioni (kwa saa za Afrika Mashariki). Sijazunguka sana kutokana na kwuasili muda huo mbaya lakini katika mizunguko michache niliyoifanya nimegundua kuwa zile taxi aina ya baloon ambazo zilikuwa zinaupamba mji huu katika miaka michache iliyopita, hazipo tena barabarabi. Hivi sasa taxi nyingi ni magari ya kawaida na nyingi ni mbovu mno.
Katika ulizauliza yangu, mtu mmoja alinifahamisha kuwa baloon zilichangamkiwa sana na watu waliokuwa wakifanya biashara ya taxi lakini baadaye wakabaini kuwa si gari imara za kuhimili kazi hiyo, wengi waliozinunua waliishia kupata hasara na sasa wanaziogopa kama ukoma. Hayo ni madhara mengine ya bidhaa feki zinazoingizwa nchini kwani nyingi ya baloon hizo zilitokea mashariki ya mbali.
Nitaendelea kuwajuvya mambo nitakayokumbana nayo mjini humu kwani nitakuwepo hadi Jumamosi Mungu akipenda.

1 comment:

Anonymous said...

Hii serikali yetu ni wapuuzi, ilipaswa kutumia mapato ya tanzanite kuwekeza kwenye mambo mengine ili itakapoisha tusihangaike. we ngoja tu,hata kwenye dhahabu na madini mengine itatokea hivyo hivyo, yaani kama tumerogwa vile