Tuesday, April 1, 2008

BREAKING NEWS: CUF yakataa kura ya maoni

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema kuwa hakitashiriki kuwafanyia wananchi usanii kama ambavyo ilivyopendekezwa na CCM. Katika kikao chake cha NEC hivi karibuni, CCM iliamua kuwa suala la kuundwa kwa serikali ya mseto huko Zanzibar.
Aidha, chama hichio kimesema kuwa imani yake kwa rais Jakaya Kikwete kuhusiana na suala la majadiliano ya kusaka muafaka wa Zanzibar imekwisha. Sasa chama hicho kimeamua kismingi kutoshiriki tena katika mchakato wa harakati hizo zilizoanzishwa na Kikwete na kuitaka jumuiya ya kimtaifa kingilia kati ili kuvinusuru visiwa hivyo kuingia katika machafuko.
Msimamo huo wa CUF umetangazwa hivi punde na katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad. Katika tamko la chama hicho, Hamad amesema kuwa CUF haikubaliani na hoja zilizotolewa na CCM za kutaka kuendeshwa kwa kura ya maoni.
CUF haikubaliani na hoja hiyo kwa sababu: “Sisi tunaona suala hilo ni mbinu chafu tu yenye lengo la kuendelea kupoteza muda ili makubaliano yaliyofikiwa yasiweze kutiwa saini na utekelezaji kuanza.”
CUF inasema kuwa kilichofanywa na CCM ni ghiliba na usanii mkubwa lakini kinafurahi kuwa hatua hiyo ya CCM imesaidia kuwaonyesha wananchi kuwa CCM haina dhamira na kulimaliza suala hilo kubwa.

(more coming later)

No comments: