Sunday, April 6, 2008

PINDA AUSHTUKIA MKATABA WA TRL

Kuna uwezekano mkubwa kuwa mkataba baina ya Serikali na kampuni ya Rites ya India kuhusu ukodishaji wa lililokuwa Shirika la reli Tanzania (TRC) nao ni wa kinyonyaji kama ilivyo mikataba ya umeme.

Lakini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameshaushtukia mkataba huo na ameeleza wazi wazi suala hilo.

Kilichomshtua Pinda na kutofautiana kwa taarifa za wakati TRC inakaribia kumaliza kazi na zilizotolewa baada ya TRL kuanza kazi.

Mathalani, Pinda anasema kuwa wakati TRC inakaribia kumaliza kazi, kulikuwa na na injia zaidi ya 90, lakini mara baada ya TRL kuanza kazi, ilieleza kuwa kuna injini takriban 50 tu. Sasa inashangaza kuwa injini nyingine zimekwenda wapi?

Kwa upande wao, wafanyakazi wa TRL walishaonyesha wasi wasi huo tangu awali na sasa wanaitumia kauli ya Pinda kushinikiza mkataba huo upelekwe Bungeni ukajadiliwe kama ulivyojadiliwa mkataba wa Richmond.

Mwekezaji huo tayari ameshakodi injini saba ambazo kama ilivyo kwa mitambo ya kuzalisha umeme, zinalipiwa capacity charge. Capacity charge ya kila injini iliyokodiwa kutoka kwa kampuni ya Rites ni sh 600,000 kwa siku, ambazo zinalipwa hata kama injini hizo hazifanyi kazi.

Wakati huo huo, wafanyakaziw a TRL waliamua kurejea kazini jana baada ya Pinda kuwaeleza kuwa serikali imeamua kumkopesha mwekezaji huyo zaidi ya sh bil. 3 zitakazotumika kulipa viwangio vipya vya mishahara kuanzia mwezi Machi hadi Julai.

Pinda aliwaeleza wafanyakazi hao kwua mwekezaji atapaswa kurejesha fedha hizo kwa sababu ni mkopo na kuwa atumie kipindi huiki ambacho serikali imemwezesha kujipanga ili kuanzia Agosti alipe mishahara hiyo yeye mwenyewe bila matatizo.

No comments: