Ule mgogoro baina ya kampuni ya reli nchini (TRL) na wafanyakazi wake huenda ukachukua sura mpya leo wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakapokutana na wafanyakazi waliogoma asubuhi hii.
Uamuzi huo wa Pinda unaonekana ni juhudi za serikali kuokoa jahazi baada ya wafanyakazi hao kumgomea wazairi wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Pofesa Juma Kapuya.
Pinda anaingilia kati suala hilo wakati watu kadhaa wakiwa wameshateseka kutokana na kukosa usafiri wa kuwarejesha makwao bada ta wafanyakazi wa TRL kugoma.
Kutoka Dodoma, ilishaelezwa kuwa baadhi ya abiria waligeuka ombaomba baada ya kuishiwa na kushindwa kuwa na fedha kwa ajili ya usafiri mbadala wa kuwafikisha makao.
aWalipokutana na waziri huyo wiki iliyopita, wafanyakazi hao, licha ya kumzomea na kumuanikizia mabango yenye ujumbe mkali kwa serikali, walimueleza wazi wazi kuwa pasipo kulipwa mishahara mipya ambayo mwajiri mwenyewe aliahidi wiki kadhaa zilizopita, hawatorejea kazini.
Sehemu ya ujumbe katika mabango hayo ulikuwa ukiilaumu serikali kwa kumkumbatia mwekezaji huyo kutoka India huku ikishindwa kutetea haki za raia wake wanaonyonywa kwa kisingizio cha uwekezaji.
Walifikia hatua ya kumzomea kapuya baada ya waziri huyo kuonyesha wazi wazi kuwa serikali ipo pamoja na mwekezaji huyo, kiasi cha kufikia hatua ya kuanza kusikiliza sababu zuilizompfanya ashindwe kulipa mishahara ambayo aliiahidi siku chache tu zilizopita.
Leo wafanyakazi hao wanaingia katika siku ya nne ya mgomo wao, wakidai kulipwa viwango vipya vya mishahara ambayo mwajiri aliahisi katikati ya mwezi uliopita. Menejiment ya TRL ilikubali kulipa mishahara hiyo baada ya wafanyakazi hao kugoma kwa siku mbili wakidai nyongeza ya mishahara.
Makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa ni mwajiri kuongeza mshahara kwa kima cha chini kutoka sh 87,000 za wakati huo hadi sh 200,000. zaidi ya hayo, mwajiri huyo aliahidi kuongeza kiwango hicho ifikapo Agosti mwaka huu.
Lakini kwa mashangao wa wafanyakazi hao, ilipofika mwisho wa mwezi wa tatu, mwajiri hakulipa viwango hivyo vya mishahara kama alivyokuwa ameahidi na jambo hilo liliwafanya wafanyakazi wampe mwajiri huyo notisi ya saa 48, ambayo ilishamalizika na wakafikia uamuzi wa kutangaza mgomo mwingine.
Kilichoshangaza zaidi, mwajiri huyo aliamua kukaa kimya aliposhindwa kulipa mishahara. Hata wafanyakazi walipomwendea na notisi, hakutoa sababu yoyote hadi aalipoitwa na waziri kapuya alipoeleza kwa mshangao kuwa anashindwa kulipa mishahara hiyo mipya kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha.
Wafanyakazi wanahoji; kama mwekezaji hakuwa na uwezo wa kifedha, kwa nini alikubali na kuahidi kulipa mishahara hiyo?
Hivi sasa, ofisi ya Kapuya imeunda kamati inayojumuisha serikali, menejiment ya TRL na wafanyakazi, kukagua hesabu zilizotolewa na mwajiri huyo, ili kuthibitisha kuwa kweli hawezi kulipa mishahara hiyo.
No comments:
Post a Comment