Thursday, April 3, 2008

Serikali yakubali kuibeba TRL

Serikali imesema kuwa ipo tayari kulipa sehemu ya mishahara ambayo mwajiri wa kampuni ya reli nchini (TRL) anapaswa kuwalipa waajiriwa wake.

Waziri wa kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Alhaj Juma Kapuya, amesema kuwa serikali itajitisha mzigo huo baada ya kuzipitia hesabu za mwekezaji huyo.

Ameyasema hayo baada ya mwekezaji huyo kubainisha kuwa hana uwezo wa kuwalipa watumishi wake mishahara wanayohitaji, licha ya yeye mwenyewe kukubali na kusaini makubaliano mapema mwezi uliopita kuwa atalipa kima cha chini cha sh 200,000 kuanzia mwezi machi na ifikapo Agosti ataongeza kiwango hicho.

Mwekezaji huo ameushangaza ulimwengu kwa kukubali kulipa kiasi hicho, lakini akashindwa kufanya hivyo bila kutoa sababu yoyote mpaka pale wafanyakazi walipogoma. Hata walipotoa tishio hilo la kugioma, mwajiri huyo hakueleza sababu ya kushindwa kulipa mishahara hiyo, zaidi ya kutabngaza kusitisha kwa safari za treni kwa muda usiojulikana.

Lakini inaelekea kuwa mwajiri huyo aliidokeza serikali kuwa haina uwezo wa kifedha kulipa mishahara hiyo na kumpelekea kapuya hesabu zao zinazoonyesha kuwa hawezi kulipa mishahara hiyo.

Hiyo inathibitishwa na kauli ya Kapuya kuwa serikali itazipitia hesabu hizo kwa kuwa zimeandaliwa na mwekezaji huyo peke yake.

Lakini kapuya ameshangaza zaidi pale alipoahidi kuwa serikali italipia sehemu ya mishahara hiyo iwapo itajiridhisha kuwa kweli mwekezaji huyo hawezi kuwalipa watumishi viwango vya mishahara ambavyo yeye mwenyewe alivikubali na kupanga muda wa kulipa!

No comments: