Thursday, May 8, 2008

BoT yaichunguza TPB

SIKU chache baada ya kuibuka kwa tuhuma za ubadhirifu ndani ya Benki ya Posta (TPB), Benki Kuu (BoT) imekiri kutuma maofisa wake kufanya uchunguzi ndani ya benki hiyo.

Ingawa alikuwa mgumu kukubali moja kwa moja kuwa BoT inaichunguza TPB, Gavana wa BoT, Profesa Beno Ndullu alithibitishia kuwa BoT imewatuma maofisa hao kufanya uchunguzi.

Akionekana kutaka kukwepa kulizungumzia suala hilo moja kwa moja, Ndullua alisema ni kawaida ya BoT kufanya ukaguzi wa mra kwa mara katika mabenki yote.

Hata hivyo, alipoulizwa inakuwaje wakati benki inakabiliwa na tuhuma kama ilivyo kwa TPB, Ndullu alisema kuwa katika mazingira hayo, ni lazima uchunguzi wa BoT uwe wa kina zaidi na usisubiri muda maalum.

Benki hiyop inachunguzwa kwa ufisadi wa mamilioni ya shilingi, udanganyifu wa baadhi ya watendaji wake na rushwa.

Tuhuma hizo zilichapishwa kwa mara ya kwanza katika mtandao wa Jambo Forusm, na kuwashtua viongozi wakuu wa benki hiyo, na Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo ambao waliunda kamati ya kuchunguza mtu aliyevujisha siri.

Habazi zilizopatikana zinadai kuwa moja kati ufisadi unaotajwa unamuhusisha Alphonce Kihwele, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo na tuhuma za kughushi barua ya bodi ya Benki ya Posta, ili kuongezewa mkataba wakati bodi inadai haikuwahi kukaa kikao kupendekeza aongezewe muda.

Mbali na tuhuma hizo, pia imeelezwa kuwa ufisadi mwingine uliofanyika unamhusisha kigogo mwingine anayedaiwa kuwalazimisha watengeneza mahesabu katika idara ya fedha kuhakikisha wanatoa hesabu zinazoonesha benki inapata faida kinyume na ukweli, hata hivyo inadaiwa kuwa Benki kuu ya Tanzania (BOT) imeweza kumbana baada ya kugundua hitilafu iliyofanywa.

Aidha, tuhuma nyingine ni zile zinazodai kuwa Mtendaji huyo ameandaa timu yake ya mtandao inayowahusisha baadhi ya wafanyakazi ndani ya benki hiyo, ili kuweza kufanikisha ufisadi huo.

Pamoja na mambo mengine, inadaiwa kuwa timu hiyo ndiyo iliyoiingiza Benki hiyo katika mikataba mibovu ikiwemo ule wa uwekaji na uendeshaji wa mashine za kutolea fedha (ATMs) ambazo zinadaiwa kuigharimu benki hiyo mamilioni ya fedha.

No comments: