Sunday, May 18, 2008

CCM, CUF watwangana

Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa Chama cha Wananchi (CUF) katika jiji la Tanga wametwangana mangumi baada ya kutokea kutoelewana baina yao katika mkutano wa kisiasa.
watu kadhaa wmejeruhiwa katika mapigano hayo, yaliyowalazimisha polisi kurusha risasi hewani ili kuwatawanya watu, yalitokea katika Barabara ya 20, wakati wafuasi wa CUF walipoandaa mkutano wa hadhara katika eneo ambalo lipo karibu na opfisi za CCM katika mtaa huo.
Taarifa zinasema kuwa CUF walipewa kibali na Polisi kufanya mkutano huo ambao ulikuwa uhutubiwe na mmoja wa viongozi wa juu wa chama hicho, said Miraji.
Mara baada ya kupata taarifa kuwa CUF watafanya mkutano katika eneo hilo, CCM nayo ilijiandaa kukabiliana na hali hiyo. Waliweka maspika makubwa katika eneo la ofisi zao na kuanza kutangaza masuala yanayohusu chama chao.
Baada ya wafuasi wa CUF kukusanyika kwa ajili ya mkutano huo, kijana mmoja mfuasi wa chama hicho, alitakiwa kupanda jukwaani ili kutoa hotuba, kabla Miraji hajakaribishwa rasmi kumwaga sera za chama hicho.
Baada ya kuona hivyo, CCM nao walimchukua baba wa kijana aliyekuwa katika jukwaa la CUF, na kumtaka aeleze masuala kuhusu CCM. lakini inaelekea katika maelezo yao, walianza kushambuliana jambo lililoamsha hasira za wanachama waliokuwa wakisikiliza hotuba hizo za baba na mwana kutoka majukwaa tofauti yaliyo jirani.

No comments: