Rais wa Zanzibar, Amani Karume, amesema hawezi hivi sasa kuwateua mawaziri katika baraza lake kutoka chama cha upinzani kwa sababu katiba hairuhusu.
Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu, alisema kuwa katiba iliyopo na mfumo wa utawalauliopo hautoi nafasi kwa yeye kuwateua mawaziri kutoka upinzani.
Alisema kuwa katika uchaguzi wa mwaka 2005, Pemba alipata kura 20,000 na waliwachagua wanaCCM wawili kuwa wawakilishi na tayari wameshaingizwa katika baraza ,a mawaziri na kuhoji hao wanaowataka wapemba waingizwe kwenye baraza watatokea wapi?
Aidha, aliwashangaa CUF kwa kukataa sualalakura ya maoni, akisema kuwa ushirikishwaji wa wananchi ni jambo muhimu ambalo linapiganiwa na kila mtu.
Aliwataka waandishiw a habari aliokuwa akizungumza nao kuwaelimisha CUF kuwa hali ya mambo haipo kama wao wanavyofikiri na kuwa madai yao ya kushirikishwa katika serikali hayana msingi kwa sababu hata sasa wanashirikishwa katika serikali kupitia baraza la wawakilishi.
Akifafanua kuhusu kura ya maoni, alisema kuwa si lazima Tume ya Uchaguzi Zanzibar isimamie kura hiyo na pia haitaubdwa tume maalum ya kuisimamia lakini akahakikisha kuwa kila Mzanzibari atashiriki kupiga kura.
Aidha, rais Karume amesema kuwa milango ya Ofisi yake ipo wazi kwa mtu yeyote mwenye shida kwenda.
Hata hivyo, alisema kuwa iwapo Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, anataka kuonana naye kama vilealivyomuomba Rais Jakaya Kikwete awakukutanishe, anapaswa kanza kumtambua yeye kuwa ni rais.
No comments:
Post a Comment