Mbunge wa Karatu, Dk. Wilibrod Slaa (Chadema) ameshinda kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akitoa hukumu ya kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, jaji Robert Makaramba alizitupilia mbali hoja zote zilizotolewa na walalamikaji hao akisema kuwa hazina msingi.
Katika kesi hiyo, walalamika walidai mahakamani hapo kuwa msimamizi wa uchaguzi huoalikiuka taratibu kadhaa ambazo zilisababisha mgombea wao, Patrick Tsere, ashindwe.
Aidha, walalamika walidai kuwa kulikuwa na kura za mgombea waozilizoibwa na iwapo angepatiwa angeweaa kuibuka mshindi.
Katika dai jingine, waliieleza mahakama kuwa Msimamizi wa uchaguzi huo hakutangaza matokeo kwa sauti kubwa, jambo lililowafanya watilie shaka matokeo yaliyotangazwa. Pia walisema kuwa msimamizi huyo alitangaza matokeo ya jumla kabla vituo vingine havijawasilisha matokeo rasmi. Walidai pia kuwa msimamizi alitumia fomu tofauti kutangaza matokeo hayo.
lakini katika uamuzi wake, Jaji Makaramba alisema kuwa hoja hizo hazina msingi kwa sababu hazionyeshi ni jinsi gani zimemuathiri mgombea aliyeshindwa.
Alisema pia kuwa suala la kuibiwa kura, lilitokea pia hata kwa Dk. Slaa na aiwapo na yeye angepewa kura alizopunjwa, kama ilivyojionyesha kwenye vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, bado angebakia kuwa mshindi hata kama mgombea wa CCM angepewa kura anazodai 3000.
Hata hivyo, Jajialikataa ombi la wakili wa utetezi, Tundu Lissu, kuomba walalamikaji na mawakili wao wafunguliwe mashitaka ya kuidanganya mahakama kwa kuleta vielelezo vya uongo mahakamani kama ilivyothibitika wakati wa kusikiliza kesi hiyo.
Jaji alisema kuwa suala la kuthibitisha nyaraka za kughushi lipo chini ya Jeshi la Polisi hivyo ni vema wakaachwa walishughulikie suala hilo na iwapo itaonekana kuwa watu hao wametenda kosa fulani, wachukuliwe hatua zinazostahili.
No comments:
Post a Comment