Ni kama vile anaandamwa na mabalaa. Huu ni mwaka wa taabu kwa Nazir Karamagi, waziri wa zamani wa Nishati na Madini aliyelazimika kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond. Hivi sasa Karamagi ameondolewa kuwa Mwenyekiti katika bodi ya Kampuni ya Kupakia na Kupakua makontena Bandarini (TICTS) ambako anamiliki asilimia 30 ya hisa.
Mabosi wa kampuni hiyo walitangaza kuwa Karamagi anaondolewa katika nafasi hiyo kama njia ya kurekebisha mahusiano mabaya yaliyopo baina ya kampuni hiyo na serikali.
Habari kutoka TICTS zinaeleza kuwa Karamagi ataendelea kubakia na hisa zake 30 lakini taarifa ambazo hazijathibitishwa zinaeleza kuwa mipango ipo mbioni kumnunua Karamagi ili kumuondoa kabisa katika kampuni hiyo.
Maelewano mabaya baina ya kampuni hiyo na serikali yalianza baada ya watu akuanza kuhoji jinsi serikali ya awamu ya tatu ilivyorefusha mkataba wa kampuni hiyo. awali, mkataba huo ulikuwa wa mkaoa 10 lakini uliongezwa kabla haujaisha na kuufanya uwe wa miaka 25.
Inaaminika kuwa Karamagi ndiye aliyewashawisho viongozi wa awamu ya tatu kurefusha mkataba huo, na tangu hapo wananchi wengi wamekuwa wakimchukulia Karamagi kama mnyonyaji kwa kuiingiza nchi katika mkataba huo ambao hautoi nafasi rahisi kwa mtu mwingine kujiingiza kwenye biashara hiyo.
Balaa la kuondolewa uenyekiti wa bodi ya TICTS kwa Karamagi, limekuja wakati bado anasubiri hatima ya 'kesi' aliyojizushia Bungeni baada ya ksuema kuwa uamuzi wa kurefusha mkataba wa TICTS ulifanywa na baraza la mawaziri.
Kwa kuwa Karamagi hakuwa mjumbe wa baraza hilo wakati mkataba unarefushwa, Bunge lilimtaka awasilishe ushahidiw a kauli aliyoitoa lakini siku chache baada alishindwa kufanya hivyo na kujitetea kuwa nyaraka za Baraza la Mawaziri ni siri hivyo ahawezi kuziwasilisha.
Spika alikataa utetezi huo na kumpa muda zaidi Karamagi ahakikishe anawasilisha utetezi wake. Imesharipotia kuwa tayari Karamagi ameshawasilisha utetezi wake na sasa anasubiri 'hukumu' yake.
No comments:
Post a Comment