Friday, May 16, 2008

Zanzibar Yatetemesha Muungano

Kile kilio cha muda mrefu cha Zanzibar kutaka nayo ipewe mgawo kutokana na mapato yanayotokana na gesi asilia na mafuta kimefanikiwa. Kufanikiwa kwa kilio hichi kumedhihirishwa kupita kikao cha kamati ya muungano,ambacho baada ya mabadiliko sasa kinashirikisha mawaziri wote kutoka pande zote mbili za Muungano.
Kikao kilichofanyika Ahamisi kilifikia makubaliano kuwa Zanzibar iwe inapata mgawo huo. Inaelekea uamuzi huo ulifikiwa siku nyingi kwani tayari serikali ilishatafuta mshauri mwelekezi atakayelichunguza suala hilo na kuipendekeza njia muafaka ya kugawana mapato yatokanayo na rasilimali hizo.
Waziri wa nchi (Muungano), Muhamed Seif Khatib, amesema kwua tayari mshauri huyo ameshaianza kazi hiyo na anatarajiwa kuwasilisha ripoti yake mwezi Agosti mwaka huu.
Kwa muda mrefu Zanzibar imekuwa ikidai mgawo wa mapato hayo kwa kuwarasilimali hizo zimaeanishwa katika Katiba ya Muungano kama mali za Muungano. Hata hivyo, rasilimali nyingine za ardhini, kama vile madini, hazihusiki katika mgawo huo kwa sabbu hazijaanishwa kwenye katiba kama ilivyo kwa gesi na mafuta.
Aidha, kikaohicho, ambacho kipo chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais, kimeafiki kuoanishwa kwa sheria za kodi baina ya Bara na Zanzibar, baada ya kubainika kuwa wafanyabiashara kutoka Zanzibar wamekuwa wakitozwa kodi mara mbili wanapoingiza bidhaa zao Bara kutokea Zanzibar.
Hata hivyo, imebainika kuwa baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) wamekuwa wakitumia mwanya huo kuwakandamiza wafanyabiashara hao na ndio maana imeazimiwa kuwa sheria za kodi zioanishwe ili iwe inatumika sheria moja tu.
Jambo jingine litakaaloangaliwa katika kuoanisha sheria ni suala la usajiri wa magari, ili kuwaondolea usumbufu watu wa Zanzibar ambao hulazimika kulipia usajiri wa magari yao upya wanapoyaleta Bara, hata kama yalishasajirliwa Zanzibar.

No comments: