Dk. Wilibrod Slaa, Mwanasiasa wa kwanza kuzitaja hadharani tuhuma zilizokuwa zinamkabili aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), marehemu Daudi Ballali, ameibuka na kutaka uchunguzi wa kina ufanyike dhidi ya kifo alichokiita cha kutatanisha cha Ballali.
Dk. Slaa anasema kuwa mazingiya kuugua, kuondoka nchini, kulazwa nje na hatimaye kifo cha Ballali, yanatatanisha na kuacha maswali mengi sana yanayohitaji majibu ya uhakika ili kuondosha wingu la wasiwasi kutokana na kifo hicho.
Dk. Slaa, ambaye ni Mbunge wa Karatu ambaye akiwa Bungeni aliwahi kuziorodhesha tuhuma dhidi ya Ballali na mkewe Anna Muganda, alisema kuwa anaamini kuwa Ballali alipelekwa Marekani kwenda kufichwa ili asitoe siri ambazo iwapo angezisema hadharani, zingewaweka pabaya viongozi wengi pamoja na serikali yenyewe.
Kwa maana hiyo, alisisitiza kuwa kifo cha Ballali, bado kinaielemea serikali, ambayo mlolongo wa matukio, unaonyesh kuwa haikuwa tayari kutoa habari za uhakika kuhusiana na mtumishi huyo wa ngazi za juu serikalini.
Alisema inashangaza kuwa kifo hichokimetokea wakati rekodi zikionyesha kuwa serikali haifahamu Ballali alikuwa wapi hasa, lakini wakati huohup kukiwa na taarifa kwa serikali hiyo hiuyo ilituma makachero wake Marekani kwenda kuchunguza nyendo za maisha ya Ballali.
Aidha, Dk Slaa alisema serikali hadi sasa haijakiri hadharani iwapo kweli iliwatuma makachero hao hasa ikizingatiwa kuwa taarifa byibgibe zilibainisha kuwa kamati iliyopewa kazi ya kuchunguza wizi wa shilingi bil 133 za EPA, nayo iliripotiwa kwenda Marekani kumhoji Ballal.
"Haiwezekani katika kipindi cha wiki moja ,akachero waende kumfuatilia Ballali, halafu katika kipindi cha wiki hiyo hiyo Kamati iende kumhoji na baadaye zikavuma taarifa kupitia katika mtandao kuwa Ballali amefariki kabla haijathibitishwa kuwa kweli amefariki.
"Hapa lazima kuna kitu fulani kimefanywa na kinafichwa ili watanzania wasikifahamu. Na ndio maana nasisitiza uchunguzi wa kina ufanyike dhidi ya kifo hiki cha kutatanisha," anasema Dk. Slaa.
No comments:
Post a Comment