Thursday, June 5, 2008

Serikali yatangaza bajeti ya 2008/2009

*Kwa jumla itakuwa ya Tr, 7.216/-
*Utegemezi kushuka kwa asilimia 8
*Afya yaongezewa, elimu na maji mh.

SERIKALI jana ilitangaza mwelekeo wa bajeti ya mwaka wa fedha 2008/09 inayofikia sh trilioni 7.216, ambazo sehemu kubwa zitapatikana kutoka katika vyanzo vya ndani.

Waziri wa Mipango na Fedha, Mustafa Mkullo, alisema jana kuwa kiwango cha utegemezi katika bajeti ijayo, kitapungua kwa kiasi kikubwa, kutokana na mipango ya serikali kuongeza makusanyo ya mapato yake.

Aalisema kuwa kiwango cha utegemezi katika bajeti hiyo, ambayo imeongezeka kutoka sh trilioni 6.06 za mwaka wa fedha unaomalizika mwishoni mwa mwezi huu, kimeshuka kutoka asilimia 42 hadi kufikia asilimia 34.

Kutokana na malengo hayo, serikali imelenga kukusanya mapato ya ndani kiasi cha sh trilioni 4.728, tofauti na mwaka uliopita ambapo makusanyo ya ndani yalikuwa sh trilioni 3.5.

Alisema katika bajeti hiyo, kiasi cha sh bilioni 1,945 kitaelekezwa kwenye miradi na mipango ya maendeleo.

Akifafanua, alisema kuwa, jumla ya mchango wa wahisani katika bajeti hiyo utakuwa ni sh trilioni 2.430, huku serikali ikitarajia kupata sh bilioni 58 kutokana na kuuza asilimia 21 ya hisa zake katika benki ya NMB.

Alisema mwelekeo wa bajeti katika vipaumbele, hautofauitiani sana na mwaka jana. Alisema serikali imedhamiria kuendelea kutekeleza vipaumbele vile vile vya mwaka jana, ili nchi iweze kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuondoa umasikini miongoni mwa wananchi wake.

“Tumeamua kuendelea na vipaumbele vya mwaka jana kwa sababu ni ilani ya uchaguzi wa CCM, lakini pia ni vizuri kuendelea navyo, ili tuweze kufikia malengo tuliyokusudia,” alisema Mkullo.

Kutokana na mchangnuo uliotolewa na Mkullo, katika vipaumbele hivyo, sekta za afya imeongezewa fungu kutoka sh bilioni 589 hadi kufikia sh bilioni 784.5 na miundimbinu nayo imeongezewa fedha kutoka sh bilioni 777.2 hadi kufikia 971.9

Hata hivyo, mgawo wa sekta ya elimu mwakani umeshuka. Mkullo alisema sekta hiyo katika bajeti ijayo imetengewa kiasi cha sh trilioni 1.2 sawa na asilimia 17 ya bajeti yote, wakati mwaka jana ilitengewa sh trilioni 1.806 ikiwa ni asilimia 18.

Kwa upande wa sekta ya kilimo, waziri huyo alisema bajeti yake imeongezeka hadi kufikia sh bilioni 438.1 sawa na asilimia 6 ya bajeti, kutoka sh bilioni 379, huku sekta ya maji ikitengewa kiasi cha sh bilioni 217, kiasi ambacho ni asilimia tatu ya bajeti. Kiasi hicho nacho kimeshuka kutoka sh bilioni 309.1, sawa na asilimia tano ya bajeti inayomalizika.

Sekta ya Nishati na Madini imetengewa sh bilioni 382 ambapo mwaka uliopita ilitengewa kiasi cha sh bilioni 354.0, matumizi maalum yaliyotengewa sh bilioni 605.8 na sekta nyingine zilizotengewa kiasi cha sh trilioni 3.2.

Kwa mujibu wa Mkullo, sekta ya maji hivi sasa imetengewa fedha kidogo kuliko mwaka wa fedha unaoisha kutokana na kukamilika kwa miradi ya maji ya Shinyanga - Kahama.

Aidha, Mkullo alisema serikali inalenga kufuta baadhi ya misamaha ya kodi, ambayo imegundua ilitolewa kwa watu wasiostahili na hivyo kuisababishia serikali kukosa mapato.

Hivyo, alisema kutokana na hatua hiyo, serikali inatarajia kupata mapato zaidi.

Alisema serikali itaendelea na msimamo wake wa kutokopa hapa nchini, ili kuiwezesha sekta binafsi kupata mikopo kwenye taasisi mbalimbali za fedha, ili kuchochea ukuaji wa uchumi.

Alisema mbali na hatua hiyo, serikali inatarajia kuongeza mara dufu kiwango cha mbole ya ruzuku iliyotolewa kwa wakulima mwaka jana, pamoja na kutoa mbegu zizalishwazo hapa nchini, ili kuongeza ufanisi katika sekta ya kilimo kwa lengo la kukabiliana na kupanda kwa bei ya vyakula duniani.

“Hatua hizi tuna uhakika kwa kiasi kikubwa ziatasadia kukuza sekta ya kilimo na hatimaye tutapata mazao ya kutosha ambayo yataiwezesha nchi kukabiliana na tishio la kupanda kwa bei ya vyakula iliyoikumba dunia hivi sasa,” alisema Mkullo.

Wakati serikali ikitoa mwelekeo huo, kamati ya Bunge ya Uchumi na Fedha imesema kiasi cha fedha kilichotengwa katika kilimo ni kidogo sana na wajumbe wake wakapendekeza angalau iwe asilimia nane au tisa ya bajeti yote.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Abdala Kigoda, alisema kutokana na mwelekeo wa uchumi wa dunia hivi sasa, ni vema serikali ikaongeza fedha kwenye sekta ya kilimo, ambayo ndiyo uti wa mgongo wa taifa.

Alisema kilimo kinawahusisha wengi zaidi ambapo huishi vijijini na hukitegemea kwa chakula na biashara, lakini kwa bahati mbaya hawapati mbembejeo za kilimo inavyotakiwa.

“Sisi tungependa serikali iongeze fedha zaidi kwenye sekta ya kilimo kwani inajumuisha watu wengi zaidi lakini pia kwa hali ilivyo hivi sasa tusipoboresha kilimo njaa itatusumbua na kuishia kuwa ombaomba wa chakula,” alisema Mkullo.

Bajeti halisi ya mwaka wa fedha wa 2008/09 inatarajiwa kusomwa Bungeni Juni 15 mwaka huu na Mkullo, kwenye mkutano wa 12 wa Bunge unaotarajiwa kuanza Juni 10.

1 comment:

Anonymous said...

I just got my new 8G 3g iphone here in Japan.And i would want to know how to send sms/text messages to my friends and families in th ePhilippines.They are not using iphone,only smart,globe,sun etc.I really need real help,not just comments.Thank you very much
[url=http://unlockiphone22.com]unlock iphone[/url]