Mawaziri wawili wa zamani, basil Mramba na Daniel Yona. leo hii wanalala katika gerezz la Keko baada ya kutekeleza matakwa ya dhamana kutokana na kesi ya kutumia vibaya madaraka yao na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Shilingi bilioni 11.752.
Mawaziri hao wa zamani waliburuzwa katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi na kusomewas jumla na mashitaka 13 yanayohusiana na mkataba wa kampuni ya kufanya ukaguzi wa dhahabu ya Alex Atewart Asseyers.
Wanadai wakuwa walitumia madaraka yao vibaya na kuingia mkataba huo kinyume cha sheria kadhaa na kuisababishia serikali hasara hiyo.
Wakati makosa hayo yanatoka, Mramba alikuwa waziri wa Fedha na Yona alikuwa waziri wa Nishati na Madini katika serikali ya wamu ya tatu.
hali ilikuwa tete mahakamani hapo jana kwani watu wengi walifika baada ya taarifa kuenea mjini kuwa mawaziri hao wamefikishwa mahakamani hapo.
Walifikishwa wakiwa katika shangingi la takukuru na kukaa katika shangingi hilo kwa muda wa takriban saa mbili kabla ya kupandishwa kizimbani.
Ingawa walionekana kuwa watulivu, lakini Yona alikuwa na kazi ya kujifuta jasho katika kipindi chote alichokuwamo ndani ya mahakama.
Wakati wanaondoka, wananchi waliwatolea uvivu na kuwazomea wakiwaita wezi... wezi... wezi...
Katika masharti ya dhamana waliyoshindwa kuyatekeleza, Mawaziri hao wa zamani walitakiwa kuweka kiasi cha shilingi bilioni 3.9 taslim kila mmoja, kuwasilisha pasi zao za kusafiria na kuwa an wadhamini wawili wanaoaminika.
kesi hiyo itatajwa tena mwezi ujao na upelelezi wake bado unaendelea.
No comments:
Post a Comment