Serikali imesema itawafukuza wanafunzo wote wa vyuo vikuu vya serikali nchini ambao hawakubalini ya sera ya uchangiaji wa elimu ya juu.
Hayo yalitangazwa jana na Naibu waziri wa Elimu ya Juu, Gaudentia Kabaka. Kabaka alisema kuwa serikali imeuagiza uongozi katika vyuo vikuu vya uume kote nchini kuwachanganua wanafunzi wanaokubalina na sera hiyo na wale wanaoipinga.
Alisema baada ya kufanya hivyo, wale wanaokubaliana warudishwe masomoni haraka na wale wanaoipinga sera hiyo wabakie majumbani kwao.
Alisema hivi sasa serikali haina uwezo wa kugharamia ada za wanafunzi wote kwa asilimia 100 kama ambavyo wanafunzi hao wanavyodai.
Alisema bajeti ya kusaidia wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka huu ni Sh bilioni 117 na iwapo serikali ikitekeleza madai ya wanafunzi kuwa serikali ilipie ada kwa asilimia 100, zitahitajika Sh bilioni 163 na serikali haina uwezo wa kupata hiyo ziada ya Sh bilioni 52.
Alisema mpango wa serikali kuwakopesha ada wanafunzi kwa mujibu wa uwezo wao, umewezesha idadi ya wabafunzi wanaonufaika kufikia 60,000 lakini chini ya utaratibu unaodaiwa na wanafunzi, kwa kutumia kiwango cha bajeti iliyopo, idadi ya wanafunzi watakaonufaika haitafikia 40,000.
No comments:
Post a Comment