Jumla ta wanafunzi saba wa vyuo vikuu nchini walikuwa wamekamatwa hadi jana mchana kutokana na kuhusishwa na migomo iliyosababisha kufungwa kwa vyuo vikuu kadhaa vya umma.
Kamatakatama hiyo ya Polisi ilianza Jumamosi ambapo wanafunzi wawili, Julius Mtatiro (kiongozi wa zamani wa daruso) na Odong Odwar (mwanafunzi rais wa Uganda ambaye anaelezwa kuwa ni mwanaharakati nzuri), walikamatwa na kuanza kuhojiwa. lakini katika hali ya kushangaza, Polisi bado haitaki kukiri kuwa inawashikilia wanafunzi hao.
Waliokamatwa wote ni viongozi wa serikali za wanafunzi katika vyuo wanavyosoma.
Wengine watano walikamatwa jana. Hao ni Rais wa DARUSO, Anthony Machibya, waziri mkuu Benedicto Raphael na waziri wa elimu wa UDSM, Suleman Ally.
Wengine waliokamatwa ni rais wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Afya Muhimbili, Godbless Charles na rais wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Cha Ardhi, Anthony Massawe.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, amesema kuwa yeye hana taarifa za kukamatwa kwa vijana hao ingawa taarifa za uhakika zimeenea mjini kuwa baadhi yao walikamatwa katika kituo cha cha Channel Ten wakati walipokuwa wanarekodi moja ya vipindi vya mahojiano vinavyoandaliwa na kurushwa na kituo hicho.
1 comment:
Kazi ipo!
Post a Comment