Friday, November 14, 2008

Mahakimu Kesi za EPA 'wagoma'

Mahakimu wanaosikiliza kesiz a watuhumiwa wa wizi wa mabilioni ya fedha za EPA, leo wasitisha kwa muda kusikiliza kesi hizo, na 'kuandamana' hadi Mahakama Kuu kuwasilisha malalamiko yao.
Malalamiko yao yanahusisha usalama mdogo na kupatiwa vitendea kazi. Msajili wa Mahakama Kuu kimsingi alikubaliana na madai hayo na kuahidi kuwa kuanzia sasa mahakimu hao watapatiwa magari kwa ajili ya kuwachukua na kuwarejesha majumbani mwao.
Walipofika asubuhi leo, walisikiliza kesi moja ambapo waliwapatia dhamana Johnson Lukaza na mdogo wake na kisha kuahirisha usikilizaji wa kesi, ili kwenda Mahakama Kuu kuwasilisha malalamiko yao.
Huko walionana na jaji Mfawidhi, ambaye aliwapeleka kwa msajili walikowasilisha malalamiko yao.
Baada ya kurejea, waliskiliza kesi moja inayomkabili jeetu Patel na wenzake na kumkubalia dhamana na kisha wakaingia tena kwenye kikao Mahakamani hapo pamoja na msajili.
baada ya kikao hicho, hivi sasa mahakimu hao wanaendelea kusikiliza kesi nyingine ya Jeetu huku wafanyakazi wa BoT ambao nao wameshitakiwa wakisubiri na wao zamu yao ya kusikiliza maombi yao ya rufaa.
lakini taarifa nyingine zinadai kuwa malalamiko ya mahakimu hao yanahisuska pia mambo ya fedha.
Mahakimu wanadai kuwa waendesha mashitaka katika kesi hizo wanalipwa posho maalum ambayo wao (mahakimu) hawapewi).
Pia wanadai kuwa kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hizo, waendesha mashitaka walipatiwa mafunzo maalum kuhusu kesi hizo wakati wao hawakupatiwa mafunzo yoyote.
lakini kubwa zaidi, habari zimeenea mitaani kuwa wanahusika katiak kesiz a EPA wamekuwa wakihongwa kiasi kikubwa cha fedha. nadhani hatua hii ya mahakimu ni kutaka kujionyesha kuwa wao si baadhi ya hao wanaodaiwa kuhongwa

No comments: