Taarifa za hivi punde kutoka Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu zinapasha kuwa wafanyakazi wanne wa BOT wamepandishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayohusiana na wizi wa pesa za EPA wa zaidi ya shilingi bilioni 207 mali ya BOT.
Waliopandishwa kzizimbani ni:
1. Bi. Esther Komu, ambaye ni Kaimu mkurugenzi wa Idara ya Madai.
2. Bosco Kimela ambaye ni Kaimu Katibu wa BoT.
3. Imani Mwakyosa, anayetajwa kuwa ni Mwanasheria na
4. Sophia Joseph (kutoka Idara ya Fedha) ambao nyadhifa zao tunaendelea kuzitafuta.
Kuna baadhi ambao waliunganishwa katika ksi nyingine zilizofunguliwa jana na juzi na wengine wamesomewa mashitaka mapya peke yao. Bado kesi zinaendelea Kisutu
Wakati hayo yakitokea, taarifa za hivi punde zinapasha kuwa Johnson Lukaza, ambaye alipandishwa mahakamani juzi, amefanikiwa kupata dhamana na ameachiwa
No comments:
Post a Comment