Mbunge wa Mbeya Vijijini, Richard Nyaulawa, amefariki dunia. Kifo cha Mbunge huyo kimethibitishwa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta.
Nyaulawa amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa kansa ya utumbo uliokuwa unamsumbua kwa muda mrefu.
Wakati fulani alipelekwa nchini India kwa matibabu lakini tangu aliporejea hali yake hakurudia kuwa ya kawaida. Kutokana na hali hiyo, uamuzi ulifikiwa kuwa arudishwe tena India kwa matibabu lakini kabla uamuzi huo haujatekelezwa Mungu ameamua kumchukua.
Fikra Jadidi inamuombea marehemu Nyaulawa apumzike mahali pema peponi na tutaendelea kumkumbuka kwa kazi zake njema alizozifanya duniani, Amen
No comments:
Post a Comment