Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Vijijini, Richard Nyaulawa, utaagwa Jumatatno jijini Dar es Salaam na kusafirishwa siku ya Alhamisi kwa ndege mbili za kukodi. Ukiwasili jijini Mbeya, mwili huo utapelekwa kijijini kwa marehemu, Inyara, ambako mazishi yatafanyika siku hiyohiyo.
Msemajiw a familia, Aga Mbughuni, amesema marehemu alipelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu ya saratani ya ini mwezi Julai mwaka huu na alirejea nyumbani wiki iliyopita.
Marehemu amecha mjane, watoto wanne na wajukuu wanne.
Nyaulawa anakuwa ni Mbunge wa sita kufariki katika Bunge hili. Wabunge wengine waliofariki ni aliyekuwa Mbunge wa Tunduru, Juma Akukweti, ambaye alifariki nchini Afrika Kusini, alikopelekwa kwa ajili ya matibabu baada ya kupata ajali ya ndege jijini Mbeya.
Wengine ni wabunge wa viti maalum, Amina Chifupa na salome Mbatia. Chifupa alifariki kwa maradhi na Mbatia katika ajali ya gari.
Baadaye alifariki Benedict Losurutia (Kiteto) kutokana na maradhi na wa mwisho kufariki kabla ya Nyaulawa ni Chacha Wangwe (Chadema-tarime) aliyefariki kwa ajali ya gari katika eneo la Pandambili mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment