Mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF) umemburuza mahakamani Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Moyo Tanzania (THI), Dk. Ferdinand Masau kwa madai kuwa kushindwa kulipa michango ya wafanyakazi wake.
Kwa mujibu wa hatu ya mashitaka ya kesi hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, dar es salaam, Dk. Masau ameshindwa kwuasilisha michango ya wafanyakazi wake inayofikia zaidi ya sh milioni 79.
Kesi hiyo, iliyofunguliwa na wakili wa NSSF, Crispine Meela, ipo mbele y Hakimu Mkazi Richard Kabate.
Hata hivyo, Dk masau hajapelekewa wito wa kuitwa shaurini ingawa kesi hiyo inajulikana kama ya jinai kwa mujibu wa sheria ya NSSF.
Hati ya mashitaka inaeleza kuwa Dk masau amekiuka kifungu cha 72 (1) (d) cha sheria ya NSSF namba 28 ya 1997. Inadaiwa kuwa Dk. Masau, akiwa kama kiongozi wa taasisi iliyosajiliwa na NSSF na kupewa namba ya uanachama 678171, alishindwa kuwasilisha michango ya watumishi wake kati ya Mei 2004 na November 2007.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, mtu anayepatikana na hatia ya kukiuka kifungu hicho anaweza kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka miwili au faini ya sh 100,000.
1 comment:
Genial fill someone in on and this fill someone in on helped me alot in my college assignement. Thanks you on your information.
Post a Comment