Zaidi ya abiria 50 waliokuwa ndani ya ndege ya Air Tanzania Company Limited iliyokuwa inaelekea kuruka katika uwanja wa Mwanza, wamenusurika baada ya rubani kufanikiwa kuisimamisha ndege hiyo kutokana na moja ya tairi kuanza kuwaka moto.
Moto huo uligunduliwa na mmoja wa abiria aliyekuwa amekaa siti za nyuma ambaye alianza kupiga kelele zilizowashitua abiria wenzake ambao nao walianza kupiga kelele kabla ta rubani kushituka na kuisimamisha ndege hiyo iliyokuwa inashika kasi ili ipae.
Mara moja askari wa zimamoto walifika na kufanmikiwa kuuzima moto huo na kuwashusha abiria wote ambaow alipelekwa kwenye vyumba vya kusubiria uwanjani hapo.
Mmoja wa abiria ameeleza kuwa tanguw awekwe hapo, hakuna ofisa yeyote wa ATCL aliyekwenda kuwaleza chochote zaidi ya kufahamishwa tu kwua safari yao imefutwa kwa leo.
Abiria huyo alisema kuwa ingawa waliripoti uwanjani hapo saa 4 asubuhi kulingana na ratiba ya wali, safari yao ilisogezwa mbele na walipanda kwenye ndege saa 8.
Mkrugenzi wa ATCL, David Mataka, alipotafutwa alisema kuwa ndio kwanza alikuwa amepata taarifa hizo na kuomba apataiwe muda ili akusanye taarifa zaidi. Alitaka apigiwe simu kama baada ya dakika 40.
Ndege iliyopata ajali hiyo ni aina ya dash 8 ambayo ina uawezo wa kubeba abiria wapata 56 na ni moja ya ndege zilizokodiwa na shirika hilo katika harakati zake za kujiimarisha kibiashara
No comments:
Post a Comment