Habari kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zinasema kuwa Basil Mramba na Daniel Yona, ambao walikuwa na matarajio ya kupata dhamana leo, wamerejeshwa tena Keko.
Mawaziri hao wa zamani, wanaokabiliwa na mashitaka 13 ya kutumia madaraka yao vibaya, walifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuomba dhamana baada ya Mahakama Kuu kutengua masharti ya awali wiki iliyopita.
Walipofikishwa Mahakamani Kisutu leo, Hakimu anayeisikiliza kesi hiyo, alikataa kuendelea nayo kwa maelezo kuwa alikuwa hajaipanga kusikilizwa leo. Pia, hakimu huyo Hezron Mwankenja, alisema kuwa yeye hakuandika removal order kulitaka jeshi la Magereza liwalete watuhumiwa hao mahakamani leo.
Baada ya kufanya hivyo, aliipangia kesi hiyo kusikilizwa kesho, hivyo kuwalazimua Mramba na Yona kurejea keko hadi hiyo kesho.
Awali, hakimu huyo alipanga dhamana iliyoelezwa kuwa na nasharti magumu, akimtaka kila mtuhumiwa kuweka mahakamani hapo kiasi cha Sk bil 3.9, kuwa na wadhamini wawili, kusalimisha hati zao za kusafiria na kutotoka nje ya dar bila idhini ya mahakama.
mahakama Kuu ilitengua sharti la kwanza na kuwataka watuhumiwa aidha kutoa kiasi cha Sh bil 2.9 au kuwasilisha hati ya mali yenye thamani hiyo.
1 comment:
Jasho litawatoka!
Post a Comment