Monday, October 26, 2009

Sarakasi za tatizo la umeme

waziri Ngeleja anaeleza kuwa hakutakuwa na ongezeko la bei ya umeme baada ya kuanza kutumika kwa mitambo ya IPTL. Anasema hivyo akijua kuwa gharama za kuitumia IPTL ni kubwa sana. Anajidanganya.
hata kama hakutakuwa na ongezeko la beo moja kwa moja itakayolipwa na mtumiaji, lakini gharama hizo kubwa ni lazima zitalipiwa na serikali. Ina maana bado fedha za walipa kodi, fedha wananchi, ndizo zitakazotumika kulipia gharama hiyo. Kwa nini Ngeleja anatudanganya kuwa hakutakuwa na ongezeko la bei wakati gharama hizo tunazilipa sisi wenyewe?

Saturday, October 24, 2009

Makali ya mgao wa umeme yaanza kupungua?

Baada ya kuhangaika na pilikapilika, hatimaye Waziri wa Nishati, William Ngeleja, alitangaza juzi kuwa umeme katika mitambo ya IPTL unaweza kuanza kupatikana Novemba Mosi. Siku hiyo hiyo kuna uwezekano pia kuwa mitambo mipya ya tanesco iliyopo Tegeta nayo itaanza kufanya kazi.
Tulitarajia kuwa jana Ijumaa, mtambo wa Songas uliokuwa umeharibika ungeanza kuingiza katika gridi ya taid kama Megawati 20 hivi. Lakini kabla haya hayajafanyika naona kama kuna nafuu fulani (au labda ni kwa upendeleo) kwa maana watu tunaoishi tangu bovu hatujakatiwa umeme tangu juzi. Ndio maana najiuliza iwapo makali ya mgawo yameanza kupungua au ni Tanesco walisahau kukata umeme katika eneo letu!

Thursday, October 22, 2009

KIkwete aingilia tatizo la umeme

Sijui kama ufumbuzi wa muda utapatikana baada ya rais Kikwete kuingilia na kutoa maagizo kwa watendaji wake kuhakikisha wanamaliza mgawo wa umeme. Hii ni taarifa ia Ikulu:

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAFANYABIASHARA na wawekezaji nchini katika kongamano la kujadili fursa za utalii nchini mjini Dar es Salaam, jana, Jumanne, Oktoba 20, 2009 walimwomba Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuingilia kati matatizo ya sasa ya mgawo wa umeme kwa kuruhusu kuwashwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa tayari Mhe. Rais ameingilia kati kumaliza mgawo wa sasa wa umeme nchini.

Tokea majuzi, Mhe. Rais alikwishakutoa maagizo kwa Wizara ya Nishati na Madini, pamoja na Kampuni ya TANESCO, kuchukua hatua za kuhakikisha mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL inawashwa, haraka iwezekanavyo, na umeme unaanza kupatikana.

Kutokana na kuharibika kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya Songas, Ubungo, mjini Dar es Salaam, na Kihansi, Mkoani Iringa, Gridi ya Taifa ina upungufu wa megawati 80, ikiwa ni megawati 20 ambazo kwa kawaida huzalishwa na Songas, na megawati 60 ambazo huzalishwa Kihansi.

IPTL kwa sasa haizalishi umeme. Lakini ina uwezo wa kuzalisha megawati 90 hadi 100. Hizi zinatosha kuziba pengo la sasa la megawati 80 katika Gridi ya Taifa, na kumaliza mgawo wa sasa wa umeme.

Ni kweli kwamba IPTL iko kwenye mchakato wa ufilisi ambao unaendelea sasa mahakamani, lakini Mhe. Rais Kikwete ameelekeza kuwa mchakato wa ufilisi mahakamani hauzii mitambo ya kampuni hiyo kuwashwa na kuzalisha umeme wakati malumbano ya kisheria yakiendelea kortini.

Katika kuhakikisha kuwa umeme unapatikana haraka iwezekanavyo, Mhe. Rais Kikwete ametoa maagizo mbalimbali kwa Wizara za Serikali kama ifuatavyo:

(a) Wizara ya Nishati na Umeme, kwa kushirikiana na TANESCO, imeagizwa kusimamisha masuala yote ya kiufundi ikiwa ni pamoja na upatikanaji haraka wa mafuta, ili umeme huo wa IPTL uanze kuzalishwa mara moja.

(b) Wizara ya Fedha na Uchumi imeagizwa kuhakikisha kuwa inatafuta fedha za kuwezesha ununuzi wa mafuta na mahitaji mengine muhimu, ili umeme uweze kuzalishwa.

(c) Wizara ya Katiba na Sheria imeagizwa kuhakikisha kuwa inasimamia masuala yote ya kisheria yanayohusu suala hilo

Katika kutekeleza maagizo hayo ya Mhe. Rais, jana, Jumanne, Oktoba 20, 2009, Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, tayari aliitisha kikao maalum cha Mawaziri wa Nishati na Madini, Fedha na Uchumi, Katiba na Sheria, TANESCO na vyombo vingine husika katika suala hilo kujadili jinsi ya kuhakikisha kuwa umeme wa IPTL unawashwa haraka.

Kupatikana kwa umeme wa IPTL utawawezesha mafundi ambao kwa sasa wanahangaika kutengeneza mitambo ya Songas na Kihansi kuifanya kazi hiyo kwa utulivu zaidi.

Mhe. Rais Kikwete anaelewa fika matatizo yanayowapata wananchi kwa sababu ya mgawo wa sasa wa umeme, na madhara yake kwenye uchumi wa nchi. Lakini anapenda kuwahakikishia wananchi wote kuwa mgawo wa sasa wa umeme utakwisha katika siku chache zijazo.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

21 Oktoba, 2009

Sunday, October 11, 2009

Swine flu claim first victim in Tanzania

Kama ilivyoandikwa na Sunday Citizen

Swine flu, reported in the country hardly three months ago, has claimed its first victim. The first death has been confirmed in Mbulu district, Manyara region where at least 35 people have tested positive to AH1N1. The district medical officer Dr. Anael Palangyo told Sunday Citizen late yesterday that the victim was one of those who had tested positive to the disease. She has been identified as Ms Elizabeth Passi, a primary school teacher in Mbulu town. She passed away on Thursday at the hospital there. He said the deceased was among several swine flu suspects and those confirmed, who had been admitted at the district hospital. He stated that although several patients were treated and discharged, her situation deteriorated before she died on October 8. ''This could be the first death of confirmed swine flu case in the country'' he said over telephone from Mbulu. Although many countriesin the region have reported cases of swine flu, the death in Tanzania may also be the first known case in East Africa. He could not rule out the possibility of the situation worsening because there are already 167 other people in the area suspected to have been infected with the disease. ''It is true we have 167 on the list of suspects. What we are doing now is to take their blood samples to Dar es Salaam for examination,'' he pointed out. Dr. Pallangyo said the victim was one of those whose blood samples have been examined and proved positive for AH1N1 at the Central Government Laboratories in Dar es Salaam. He added that out of 27 samples whose results were returned to Mbulu medical authorities last Thursday, 20 tested positive for swine flu. Fifteen other people tested positive in other samples examined and received at Mbulu district hospital on September 30th. More samples are being sent for examination. According to him, most of the swine flu patients and suspects were traced in and around Mbulu town and very few from distant villages. He further noted that it had been difficult to differentiate swine flu and other types of fevers, necessitating taking blood samples to Dar es Salaam for examination. ''Swine flu has more or less similar symptoms with other fevers. That is why we have to ensure proper detection through blood screening,'' he said, adding that there was not proper facility to do this elswhere in the country. A total of 170 H1N1 cases had been recorded in the country by September, according to a report by the Ministry of Health and Social Welfare. Permanent Secretary Ms. Blandina Nyoni said Dar es Salaam Region has recorded the highest number of swine flu cases followed by Manyara and Mara regions. At the end of September, Dar es Salaam had recorded 151 cases, most of them in boarding schools, Manyara 15 and Mara four. According to the report, out of the 170 cases, 80 are Tanzanians and 90 were foreigners. The government warned that the increasing number of swine flu cases was an indication that the disease might spread more if tangible measures were not taken to control it. The first swine flu case in the country was reported last July when a 17-year old British student, among 15 students and teachers who had flown from Britain via Kenya for a volunteer work, tested positive. The disease has also been reported in Kenya and Uganda, prompting the East African Community to issue an alert notice to its member states. To date, 24 countries in Africa have been proved to have the disease with over 8,187 cases and 41 deaths recorded. South Africa is leading with a high number of cases: 7,606 patients and 31 deaths. Globally, H1N1 flu has infected more than 94,000 people, including 429 deaths, according to the World Health Organization. First reported on April 23 this year in Mexico, the human cases of A/H1N1 influenza has so far spread to many nations. In Mbulu, The first swine flu case was confirmed on September 22 but it was only until three days ago that the first death was reported. As is the case in other regions, medical officers in Mbulu have linked the oubreak of the disease to students returning to the area from vacation. ''I cannot say how swine flu was spread there. Most of us guess they could have been brought in by students returning from vacation in Dar es Salaam, Arusha, Mwanza and other places,'' he said. However, the DMO allayed fears that the situation could get out of hand, saying swine flu was not that deadly disease because it can be treated if detected early. Measures being taken by the district authorities is to sensitize the public to report to medical facilities people with symptoms associated with AH1N1. When contacted to comment on the situation, the Manyara regional commissioner Henry Shekiffu confirmed to have heard of the death and the epidemic in Mbulu. In neighbouring Arusha, the regional medical officer Dr. Salash Toure when contacted could not confirm if the disease has been detected in the region which a high number of foreign visitors.

Friday, October 9, 2009

Ajali yaua wanane Geita

Taarifa kutoka Geita mkoani Mwanza zinasema kuwa watu wanane wamefariki baada ya magari mawili (saloon) kugongana uso kwa uso. Magari hayo, ambayo huko Geitwa ni maarufu kama vipanya (na si Toyota Hiace kama ilivyozoeleka kuitwa mijini hasa Dar), yanatumika kama mabasi ya abiria.
Inadaiwa kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi. Kati ya waliofariki ni deremo wa mmoja wa magari hayo. Dereva mwingine ameshakimbia

Obama wins Nobel Peace Prize

Hii nimeitoa Reuters;

U.S. President Barack Obama won the Nobel Peace Prize on Friday for giving the world "hope for a better future" with his work for peace and calls to reduce the global stockpile of nuclear weapons.

The Norwegian Nobel Committee praised Obama for "his extraordinary efforts to strengthen international diplomacy and cooperation between peoples."

The first African-American to hold his country's highest office, Obama has called for disarmament and worked to restart the stalled Middle East peace process since taking office in January.

"Very rarely has a person to the same extent as Obama captured the world's attention and given its people hope for a better future," the committee said in a citation.

It awarded the prize to Obama less than nine months into his presidency. Despite setting out an ambitious international agenda, he has yet to score any breakthrough on the Middle East or Iran's nuclear program, and faces difficult choices on the conduct of the war in Afghanistan.

Thursday, October 8, 2009

Afya ya rais

Mapema leo asubuhi, Madaktari wa rais Jakaya Kikwete walikutana na waandishi wa habari na kutoa taarifa kuhusiana na hali ya afya ta Mkuu wa nchi. Na hii ndio taarifa yao rasmi:



DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIATelephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425[IMG]file:///C:/DOCUME%7E1/user/LOCALS%7E1/Temp/msohtml1/01/clip_image002.jpg[/IMG]
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIMimi naitwa Dk. Peter Mfisi, ni mmoja wa madaktari wa Mhe. Rais. Nipo Ikulu. Nimekuwa na Mhe. Rais tangu wakati wa kampeni mwaka 2005 mpaka sasa. Mwenzangu ni Dk. Mohamedi Janabi ambaye ni daktari bingwa wa maradhi ya moyo katika Hospitali Kuu ya Taifa Muhimbili.Nimewaiteni waandishi wa habari kufafanua masuala muhimu kuhusu afya ya Mhe. Rais kufuatia tukio la Jumapili iliyopita, Oktoba 4, 2009, pale Mwanza. Tukio hilo limeleta mshtuko kwa watu wengi na kuendelea kuwa jambo linalozua mjadala kuhusu hali ya afya ya Mhe. Rais. Naelewa sababu ya wananchi kuwa na hofu na kuwapo kwa mjadala miongoni mwao. Rais ndiyo kiongozi wetu mkuu katika taifa na hivyo kuwa mwenye afya njema ndiyo matakwa ya kila mwananchi.Naelewa fika kuwa kutokana na kiapo changu cha udaktari na maadili yangu ya kazi siruhusiwi kutoa hadharani undani wa habari yoyote inayohusu mgonjwa ninayemtibu bila ridhaa yake.Hata hivyo, kwa kuwa huyo ni Rais wa nchi, na suala la afya yake ni kwa maslahi ya taifa na umma wa Watanzania kwa jumla, na kwa kuwa yeye ameridhia kutolewa kwa habari za afya yake ili watu wajue ukweli na kuondoa hofu, nimeamua kufanya hivyo.Kama sote tujuavyo, Jumapili iliyopita, Oktoba 4, 2009 mwaka huu, Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa anashiriki katika sherehe za miaka 100 ya Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, aliishiwa nguvu na kulazimika kwenda kwenye chumba cha mapumziko.Baada ya mapumziko ya dakika 10 hivi, Mhe. Rais alirejea kwenye shughuli hiyo na kuendelea kushirikiana na waumini wa AICT hadi mwisho wa ratiba yake.Ninapenda kusisitiza kuwa tukio la Mwanza limetokana na Mhe. Rais kuzidiwa na uchovu, na wala siyo kwa sababu nyingine yoyote ya kiafya. Wakati tukio hilo linatokea nilikuwepo, nilichukua vipimo muhimu kama daktari anavyotakiwa kufanya linapotokea tukio kama lile kwa mtu. Vipimo vyote vilithibitisha kuwa Mhe. Rais hakuwa na matatizo yoyote ya kiafya ambayo yangeweza kuhusishwa kuwa chanzo cha tukio lile.Pressure yake ilikuwa 130/85mmhg ambayo ni kiwango cha kawaida kwa mtu wa umri wake. Mapigo ya moyo wake yalikuwa 76 kwa dakika ambayo pia ni ya kawaida. Sukari kwenye damu ilikuwa 5.5mmol/l ambayo nayo ilikuwa ya kiwango cha kawaida. Joto la mwili lilikuwa digrii 37.5 centigrade ambalo ni la kawaida. Mhe. Rais pia hakuwa na kiungo chochote kilichoonekana kutetereka, jambo ambalo lilithibitisha kuwa hakupata kiharusi.Kutokana na matokeo hayo, sikuona hatari yoyote ya yeye kuendelea kushiriki katika sherehe hiyo muhimu kwa wakati huo. Ndiyo maana niliruhusu aendelee kushiriki sherehe zile mpaka alipomaliza na kuondoka.Baada ya kurudi Dar es Salaam siku ile niliwasiliana na madaktari wanzangu wa hapa nchini na nje ya nchi ambao tumekuwa tunashirikiana nao katika kuchunguza na kufuatilia afya ya Mhe. Rais. Wote hao baada ya kuwasimulia kilichotokea na matokeo ya vipimo nilivyomfanyia Mhe. Rais, kwa tafakuri zao hawakuwa na wasiwasi wowote kuwa tukio hilo lilisababishwa na jambo jingine lolote, isipokuwa uchovu. Imani yao inatokana na ukweli kuwa wanaifahamu vizuri hali ya afya ya Mhe. Rais kwa kuwa wanahusika katika kuifuatilia mara kwa mara. Mmoja wao alimuona Mhe. Rais siku moja kabla ya kuondoka New York ambapo alipata nafasi ya kuchunguza afya yake.Mimi na mwenzangu Dk. Mohammed Janabi, ndiyo wenye dhamana ya kuiangalia afya ya Mhe. Rais Kikwete kila siku. Tumekuwa tunafanya hivyo kwa zamu na wakati mwingine kwa pamoja, inapobidi kufanya hivyo. Katika kufuatilia hali ya afya ya Mhe. Rais tumekuwa pia tukimfanyia uchunguzi wa afya yake kwa vipindi maalum hapa nchini na nje ya nchi kwa vipimo ambavyo hapa nchini havipo. Napenda kuwahakikishia wananchi wenzagu kuwa katika miaka hii minne Mhe. Rais wetu amefanyiwa uchunguzi wa kina wa afya yake. Nadiriki kusema kuwa hakuna kipimo ambacho hatujapata kukifanya katika uchunguzi wa mambo muhimu ya afya yake. Kwa sababu ya kuwatoa hofu wananchi na kwa vile mwenyewe anaridhia tufanye hivyo napenda kuwapa ufafanuzi kuhusu hali ya afya ya Mhe. Rais. Katika hali ya kawaida nisingefanya hivyo kwa sababu maadili ya kazi ya udaktari yanakataza. Naamini madaktari wenzangu wataelewa mazingira niliyokuwa nayo. Katika kufuatilia afya ya rais tumekuwa tunaangalia na kuchunguza mambo yafuatayo.(a)Blood Pressure: Tunafuatilia kwa karibu sana hali ya nguvu ya msukumo wa damu (blood pressure). Tunampima mara kwa mara na mwenyewe tumempa mashine ya kujipima kila siku na anafanya hivyo. Kwa jumla pressure yake iko kwenye viwango vya kawaida. Aidha, uzito wake wa mwili unaendena ipasavyo na urefu wake. Mhe. Rais ni mtu mwenye mazoea ya kufanya mazoezi na yuko makini katika chakula anachokula. Sisi tunahusika kwa ukamilifu na kuelekeza kuhusu chakula anachokula. Hatuna matatuzi na Mhe. Rais kwa jambo hilo. Ana nidhamu ya kujipima pamoja na mazoezi na chakula. (b)Moyo: Tumekuwa tunafuatilia kwa karibu hali ya afya ya moyo wake. Tumemfanyia vipimo kama vya ECHO, ECG na vinginevyo, na hatujabaini kuwepo tatizo lolote.(c)Ubongo: Mwaka uliopita, 2008, Mhe. Rais tulimfanyia uchunguzi wa afya ya ubongo wake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hapa Dar es Salaam. Tulitumia kipimo cha CT – Scan na matokeo yameonyesha kuwa hana matatizo.(d)Ini, Figo, Bandama, Kongosho: Mhe. Rais Kikwete kila mwaka tunapomfanyia uchunguzi wa jumla wa afya yake tumekuwa tunamfanyia kuchunguza viungo vyake muhimu vya tumboni kama vile ini, figo, bandama na kongosho. Tumekuwa tunafanya hivyo kwa kutumia kipimo cha ultra sound na kwa kupima damu yake kwa kutumia vipimo muhimu. Uchunguzi huo umebaini kuwa viungo vyote hivyo ni salama na vinafanya kazi vizuri.(e)Mfumo wa njia ya Chakula: Mfumo mzima wa njia ya chakula (alimentary canal), yaani koromeo la chakula, tumbo, utumbo mdogo na utumbo mkubwa nao tumeufanyia uchunguzi wa kina kama kuna tatizo lolote katika kipindi cha miaka miwili hii. Mwaka 2007, tulimfanyia kipimo cha colonoscopy mjini Paris, Ufaransa, kuchunguza hali ya afya ya utumbo mkubwa. Matokeo ya uchunguzi yalionyesha kuwa utumbo wake mpana uko salama kabisa na hakuna matatizo yeyote. Daktari bingwa aliyemfanyia uchunguzi huo ameshauri kuwa Mhe. Rais hahitaji kufanya kipimo hicho tena mpaka baada ya miaka saba. Nakumbuka pia daktari huyo alimtania Mhe. Rais kuwa angefurahi kuazima utumbo wake. Wiki mbili zilizopita, Mhe. Rais akiwa mjini New York, Marekani, alifanyiwa kipimo cha endoscopy kuchunguza kuanzia koromeo la chakula, tumbo, na utumbo mdogo. Matokeo ya uchunguzi huo yametoa majibu mazuri kuwa yako salama. Makusudio ya kufanya vipimo hivi viwili ni kuchunguza maradhi ya kansa na viashiria vya ugonjwa huo. Bahati nzuri hana maradhi hayo na wala hakuna dalili yoyote iliyoonyesha kuwapo viashiria vya kansa.(f)Tezi la Shingo (Thyroid Glands): Aidha, wakati wa safari yake hivi karibuni majuzi mjini New York, Marekani, Mhe. Rais tulimfanyia uchunguzi wa afya ya tezi la shingo pamoja na kiwango chake cha utoaji wa homoni. Matokeo ya vipimo vyote vilivyofanyika yameonyesha kuwa hakuna matatizo yoyote.(g)Tezi la Kibofu (Prostate): Septemba, mwaka huu, 2009, tulifanya uchunguzi wa hali ya afya ya tezi la kibofu (prostate) kwa kutumia mashine maalum na kwa kuchunguza damu yake. Vipimo vyote hivyo vimeonyesha hali si mbaya. Tezi lake lina ukubwa wa kawaida na hata vipimo vya viashiria vya kansa ya tezi hilo (PSA) tunavyofanya kwenye damu vilikuwa katika kiwango cha kawaida. Mhe. Rais hana matatizo ya prostate.(h)Macho, Masikio na Pua: Tumeshamfanyia vipimo vya macho, masikio na pua na vyote viko salama. Mhe. Rais anavaa mawani lakini hayo si maradhi. Watu wengi baada ya kufikia umri wa miaka 40 si ajabu huhitaji mawani. Tunapofanya uchunguzi wa macho, ukiacha ile ya kuchunguza uwezo wa kuona, tunaangalia pressure ya macho na hali ya viungo vya nje na ndani ya jicho. Mhe. Rais hana matatizo yoyote.(i)Damu: Tumekuwa tunamfanyia Mhe. Rais uchunguzi wa damu yake kwa vipimo mbalimbali vinavyotumika kutambua maradhi mbalimbali yahusuyo damu yenyewe na mwili mzima wa mwanadamu. Tumekuwa tunafanya hivyo kila baada ya miezi sita au panapojitokeza ulazima wa kufanya hivyo. Tumekuwa tunafanya hivyo hapa nchini na hata nchi za nje kwa nia ya kulinganisha matokeo yetu na kwa vipimo ambavyo sisi hatunavyo. Matokeo ya uchunguzi wetu yameonyesha kuwa Mhe. Rais yuko salama. Hana maradhi ya damu au kisukari, wala ukimwi, au ya wingi wa mafuta (cholesterol), ama ya kiwango cha madini, au ya tezi la kibofu, wala ya tezi la shingo, au ya ini, au ya homoni mbalimbali zilizoko mwilini na mengine n.k. Jambo pekee linalojitokeza ni kwamba Mhe. Rais ana damu nyingi. Hivyo, tumekuwa tunamshauri kupunguza damu kwa kuchangia Benki ya Damu. Tunashukuru amekuwa anafanya hivyo karibu kila baada ya miezi sita. Damu nyingi inaweza kuwa na madhara mwilini lakini Mhe. Rais hajafikia kiwango cha kuwa ni tatizo la kiafya. Pia tunamshukuru kwa kuwa mwepesi kukubali kupunguza damu ambayo tunaitumia kuokoa maisha ya watu wengine. Hakuna hofu yoyote.Napenda kusema wazi watu wote wasikie na kwa ukweli kwamba mimi na daktari mwenzangu yaani Dr. Mohamed Janabi hali ya afya ya Rais silo jambo linalotutia shaka wala kutusumbua au kutunyima usingizi. Tatizo pekee ambalo limekuwa likimsumbua Mhe. Rais mara kwa mara ni maumivu ya shingo yanayotokana na kuumia zamani utotoni na wakati wa ujana. Kuumia huko ni kwa baadhi ya pingili za uti wa mgongo, sehemu ya shingo (cervical spine), kuathirika na kumsababishia maumivu. Mara nyingi matatizo ya namna hiyo huwapata wanamichezo na wanajeshi. Kutokana na shughuli wazifanyazo. Kuumia siyo jambo la kustaajabisha.Tutakumbuka kuwa Mhe. Rais amekuwa mwana michezo hususan mchezaji wa basketball, mpira wa miguu na hata riadha wakati wa ujana wake. Pia alikuwa mwanajeshi. Ili kutambua vizuri tatizo la shingo ili tujue namna ya kumpatia tiba tumeshamfanyia vipimo vyote muhimu vya uti wa mgongo toka juu mpaka chini. Tumetumia x-ray, CT – Scan na MRI-Scan. Pia ameshaonwa na madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu hapa nchini na nje. Pamoja na kuwepo athari katika shingo, madaktari hao kwa dhati wameshauri kuwa kwa sasa maumivu yake hayahitaji upasuaji isipokuwa mazoezi ya viungo. Mhe. Rais amefundishwa mazoezi anayotakiwa kuyafanya na amekuwa anayafanya kwa nidhamu ya hali ya juu. Matokeo yake ni kupata nafuu kubwa. Ndiyo maana siku hizo haonekani kunyoosha shingo mara kwa mara kama ilivyokuwa zamani kwa wale wanaokumbuka. Tunafuatilia kwa karibu sana hali ya shingo yake. Tunamfanyia vipimo vya MRI na kuonana na madaktari bingwa mara kwa mara.
MwishoNapenda kabla ya kumalizia nisisitize tena kwa kusema kuwa mimi na daktari mwenzangu hatuna mashaka na hali ya afya ya Mhe. Rais. Afya yake ni nzuri, hana maradhi yanayotishia maisha yake au kupunguza uwezo wake wa kulitumikia taifa na watu wake. Pia maoni yetu hayo ndiyo maoni ya madaktari wa ndani na wa nje waliowahi kuhusika na uchunguzi wa afya yake.Napenda pia kuwahakikishia kuwa, sisi madaktari wake, hatutachoka kufuatilia kwa karibu na kwa umakini mwenendo wa afya ya Mhe. Rais ili tujue mapema kama kuna jambo la kushughulikia. Kwa hili lililotokea, tutaendelea kuchunguza kama jambo lolote lililojificha ambalo hatujalibaini. Kwa sasa napenda kurudia kusema kuwa hakuna ushahidi wa kitaalamu wa kusema kuwa kulikuwa na sababu nyingine zaidi ya uchovu. Rais aliondoka New York Septemba tarehe 30 saa nane ya usiku kwa saa ya hapa Dar es Salaam kuanza safari ya kurudi nyumbani. Aliwasili nyumbani saa saba ya usiku wa tarehe 1 Oktoba. Njiani alisimama London na Nairobi kuunganisha ndege. Hivyo basi, alisafiri saa 24 bila ya kulala vizuri. Isitoshe hata kwenye ndege alitumia muda mwingi akifanya kazi. Asubuhi na mapema siku ya Oktoba 2, aliondoka Dar es Salaam kwenda Arusha kufungua mkutano wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola saa nne asubuhi. Baadae jioni yake alishiriki kwenye hafla ya chakula cha jioni alichowaandalia wabunge. Rais aliondoka saa sita usiku kwenda kulala. Hatuna hakika alilala saa ngapi kwani najua akiwa na kazi huchelewa sana kulala. Tarehe 3 Oktoba, 2009 alikuwa na mikutano mfululizo na viongozi na wananchi pale Arusha kabla ya kuondoka majira ya alasiri kwenda Mwanza. Alipofika Mwanza alikuwa na mazungumzo na wenyeji wake usiku ule mpaka saa nne ya usiku. Tulipofuatilia tuligundua kuwa hata siku hiyo nayo alichelewa sana kulala kwani walipondoka wageni wake yeye aliendelea kushughulikia hotuba yake mpaka karibu na alfajiri. Katika mazingira hayo kupata matatizo ya mwili kuchoka sana, na hata kukataa kuendelea kutumika, na kutaka kupumzika kama ilivyotokea si jambo la ajabu. Mwisho kabisa napenda kuwahakikishia kuwa Rais yuko salama. Afya yake ni nzuri na haina shaka yoyote. Uchovu uliokithiri ndicho chanzo cha yaliyotokea Mwanza siku ile ya tarehe 4 Oktoba, 2009. Mimi na wenzangu katika Ofisi Binafsi ya Rais (OBR) tumejifunza na tumeazimia kuwa waangalifu zaidi katika kupanga ratiba ya kazi ya Rais.Dr. Peter Mfisi Ikulu, Dar es SalaamDaktari wa Rais 08 Oktoba, 2009

I am back

It has been long time since I have posted anything here as records show. That was due to factors beyond my control. But I am now back and I will try my level best to ensure that this site is updated on hourly basis with a lot of breaking news and analysis.