Saturday, December 13, 2008

Generali Mboma ajitosa ubunge Mbeya Vijijini

Mkuu Meshi ya ulinzi mstaafu Generali Robert Mboma amechukua fomu kuomba kugombea ubunge wa jimbo la Mbeya vijini huku akikanusha kuwa ametumwa na rais Kikwete kuwnia nafasi hiyo.

Anasema kugombea ubunge ni haki yake na kugombea nafasi hiyo yamekuwa ni maamuzi yake binafsi, hivyo isihesabiwe kuwa ameingia baada ya kushawishiwa na mtu yeyote.

Alisema anagombea nafasi hiyo si kwa ajili ya kutafuta utajiri, bali kuwasaidia wananchi wenzake wa mkoa wa Mbeya kuleta maendeleo.

Alisema kipaumbele chake kitakuwa ni kutatua kero za muda mrefu zinzowakabili wananvhi wa jimbo hilo kama vile ukosefu wa maji na huduma nyingine za jamii.

"Hakuna masilahi yoyote ambayo yamenishawishi kugombea nafasi hii kwani baada ya kustaafu nilipata kiiinua mgongo changu ambacho kinanitosheleza katika kuendesha maisha yangu hivyo nia yangu ni kuwakilisha mawazo, fikra na kero za wananchi ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo katika jimbo langu la Mbeya vijijini," alisema.

Hadi Ijumaa jioni, jumla ya wanachama tisa walikuwa wameshachukua fomu hizo. Hao ni Mchungaji Luckson Mwanjali, Michael Mponzi,Jjovita Diyami, Flora Mwalyambi, Alaan Mwaigaga, Petro Mwashusa, Maria Mwambanga na Andrew Sayila .

Tuesday, December 9, 2008

Waziri Chibulunje apata ajali

naibu Waziri wa Miundombinu, Ezekia Chibulunje amepata ajali leo mkoani Singida baada ya gari lake kupinduka mara tatu baada ya tairi kupasuka. Walioshuhudia ajali hiyo wanasema Chibulunje, ambaye alipata mshituko wa moyo na majeraha madogo madogo, aliokolewa na mifuko ya hewa (airbags).
Ajakli imetokea eneo la Misugha, yapata kilometa 45 kutoka Singida mjini. Alikuwa ndio kwanza amewasili mkoani humo wka ajili ya ziara ya siku nne ya kukagua barabara akitokea mkoani Manyara. Kwenye gari lake alikuwamo na dereva na Meneja wa tanroads mkoa wa Singida ambao nao wamepata majeraha madogo na kutibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani

Friday, December 5, 2008

Serikali yatangaza mapambano na Mengi

Kauli iliyotolewa na Reginald Mengi siku mbili zilizopita imezua malumbano makali baina yake na serikali ambayo yasipoangaliwa yanaweza kuzusha migogoro isiyo na maana.
katika kile kinachoonekana kujitu tuhuma za Mengi kuwa anatishiwa na 'Wziri kijana' anayeongoza 'wizara nyeti'. Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, leo amempa Mengi siku saba kuthibitisha madai yake kuwa anatishiwa.
Waziri Masha amesema iwapo Mengi atashindwa kuthibitisha hivyo baada ya siku sana "sheria itachukua mkondo wake."
Kwa kauli hiyo, ni dhahiri kuwa serikali inaweza kumfungulia Mengi mashitaka ingawa hadi sasa ni vigumu kutabiri yatakuwa mashitaka gani hasa.
Aidha, masha alisema kuwa ameliagiza Jeshi la Polisi kuchunguza vitisha alivyopatiwa Mengi. Amemtaka mfanyabishara huyo anayemiliki vyombo vingi vya habari kuziwasilisha meseji za vitisho anazodai kutumiwa.
Siku mbili zilizopita, Mengi aliwaeleza waandishi wa habari kuwa kuna waziri alikuwa amekula njama, akitaka yeye (Mengi) amambikiziwe kodi kubwa, ili akishindwa kuilipa afilisiwe kama ilivyotokea kwa tajiri mmoja huko Urusi.
Aidha, mengi aliwaonyesha waandishi wa habari baadhi ya meseji za vitisho alivzotumiwa

Wednesday, December 3, 2008

Abiria ATCL wanusurika

Zaidi ya abiria 50 waliokuwa ndani ya ndege ya Air Tanzania Company Limited iliyokuwa inaelekea kuruka katika uwanja wa Mwanza, wamenusurika baada ya rubani kufanikiwa kuisimamisha ndege hiyo kutokana na moja ya tairi kuanza kuwaka moto.
Moto huo uligunduliwa na mmoja wa abiria aliyekuwa amekaa siti za nyuma ambaye alianza kupiga kelele zilizowashitua abiria wenzake ambao nao walianza kupiga kelele kabla ta rubani kushituka na kuisimamisha ndege hiyo iliyokuwa inashika kasi ili ipae.
Mara moja askari wa zimamoto walifika na kufanmikiwa kuuzima moto huo na kuwashusha abiria wote ambaow alipelekwa kwenye vyumba vya kusubiria uwanjani hapo.
Mmoja wa abiria ameeleza kuwa tanguw awekwe hapo, hakuna ofisa yeyote wa ATCL aliyekwenda kuwaleza chochote zaidi ya kufahamishwa tu kwua safari yao imefutwa kwa leo.
Abiria huyo alisema kuwa ingawa waliripoti uwanjani hapo saa 4 asubuhi kulingana na ratiba ya wali, safari yao ilisogezwa mbele na walipanda kwenye ndege saa 8.
Mkrugenzi wa ATCL, David Mataka, alipotafutwa alisema kuwa ndio kwanza alikuwa amepata taarifa hizo na kuomba apataiwe muda ili akusanye taarifa zaidi. Alitaka apigiwe simu kama baada ya dakika 40.
Ndege iliyopata ajali hiyo ni aina ya dash 8 ambayo ina uawezo wa kubeba abiria wapata 56 na ni moja ya ndege zilizokodiwa na shirika hilo katika harakati zake za kujiimarisha kibiashara

Tuesday, December 2, 2008

NEWS UPDATE: Mramba, Yona nje

Mawaziri wa Zamani, Basil Mramba na Daniel Yona, leo wameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusota gerezani kwa muda wa wiki moja.
Vigogo hao walipata dhamana baada ya kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga masharti magumu waliyowekewa na Mahakama ya Kisutu na jaji Njengafibili Mwaikugile alilegeza masharti hayo. Mahakama ya Kisutu iliwataka watuhumiwa hao kutoa dhamana ya fedha taslimu kiasi cha sh bil 3.9 kila mmoja.
Mahakama kuu ilibadili sharti hilo na kupunguza kiwango cha fedha hadi sh bil 2.9 na kuwaruhusu kuweka hati za mali zenye thamani kama hiyo.
Lakini Mahakama Kuu iliachia masharti mengine kama yalivyo. Nayo ni kuwasilisha pasi zao za kusafiria, kutotoka nje ya dar es Salaam bila idhini ya Mahakama na kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika.
Mramba aliwasilisha hat tatu ambazo zilikuwa na thamani ya zaidi ya sh bil 3 zenye majina tofauti, hyuku moja tu ikiwa na jina lake. Yona aliwasilisha hati tatu za thamani ya zaidi ya sh bil 3 zote zikiwa na majina yake.
Katika serikali ya awamu ya Tatu, Mramba alikuwa waziri wa fedha na Yona waziri wa Nishati na Madini. Wanatuhumiwa kutumia madaraka yao vibaya wakiwa mawaziri kwa kuingia mkataba ya kampuni ya ukaguzi wa dhahabu ya Alez Sterwat kinyume na sheria ya manunuzi na kuisababishia serikali hasara ya sh bil 11.7

Monday, December 1, 2008

Mramba na Yona warejeshwa rumande

Habari kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu zinasema kuwa Basil Mramba na Daniel Yona, ambao walikuwa na matarajio ya kupata dhamana leo, wamerejeshwa tena Keko.
Mawaziri hao wa zamani, wanaokabiliwa na mashitaka 13 ya kutumia madaraka yao vibaya, walifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuomba dhamana baada ya Mahakama Kuu kutengua masharti ya awali wiki iliyopita.
Walipofikishwa Mahakamani Kisutu leo, Hakimu anayeisikiliza kesi hiyo, alikataa kuendelea nayo kwa maelezo kuwa alikuwa hajaipanga kusikilizwa leo. Pia, hakimu huyo Hezron Mwankenja, alisema kuwa yeye hakuandika removal order kulitaka jeshi la Magereza liwalete watuhumiwa hao mahakamani leo.
Baada ya kufanya hivyo, aliipangia kesi hiyo kusikilizwa kesho, hivyo kuwalazimua Mramba na Yona kurejea keko hadi hiyo kesho.
Awali, hakimu huyo alipanga dhamana iliyoelezwa kuwa na nasharti magumu, akimtaka kila mtuhumiwa kuweka mahakamani hapo kiasi cha Sk bil 3.9, kuwa na wadhamini wawili, kusalimisha hati zao za kusafiria na kutotoka nje ya dar bila idhini ya mahakama.
mahakama Kuu ilitengua sharti la kwanza na kuwataka watuhumiwa aidha kutoa kiasi cha Sh bil 2.9 au kuwasilisha hati ya mali yenye thamani hiyo.